Saturday, June 16, 2012

TAIFA STARS YAWASILI MAPUTO

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen (kulia) akiwaongoza wachezaji wa wa timu hiyo kuelekea kwenye basi baada ya kuwasili mjini Maputo, Msumbiji.

TUMESHAPAZOEA HUKU.... Mshambuliaji Thomas Ulimwengu (katikati) akipiga mpira huku akishuhudiwa na kocha Kim Poulsen nyuma yake wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mjini Maputo, Msumbuji.


MAPUTO, Msumbiji
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, iliwasili mjini Maputo saa 5 asubuhi kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji (The Mambas) na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu.

Stars yenye kikosi cha wachezaji 20 chini ya kocha Kim Poulsen imefikia katika hoteli ya 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambapo mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa sawa na saa 10 kamili kwa saa za Tanzania.

Kwa mujibu wa programu ya kocha Kim, timu itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Mpaka timu inawasili hapa hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo yanayoweza kumfanya asicheze mechi ya Jumapili.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Maputo

No comments:

Post a Comment