Saturday, June 16, 2012

P Square waimba na Rick Ross
Mapacha wa P-Square, Peter na Paul Okoye wakifanya video ya wimbo wao waliomshirikisha rapa Rick Ross (katikati).


KUNDI la muziki la Nigeria la P-Square linaelekea kutawala dunia hivi karibuni.

Baada ya kusaini mkataba wa kufanya kazi chini ya lebo ya kurekodi muziki ya Konvict Music ya Akon, kumshirikisha Akon mwenyewe kwenye 'Chop My Money' na kuripotiwa kununua ndege binafsi, mapacha hao wamefanya ngoma mpya na rapa mshindi wa tuzo za Grammy, Rick Ross.

Mapacha Peter na Paul Okoye wameachia wimbo huo mpya uitwao "Beautiful Onyinye" pamoja na video yake inayowaonyesha wakijiachia kwenye boti ya kifahari wakimwimbia kumsifu kimwana mrembo.
 
Kutoka kwa wimbo huo kumefanya mauzo ya albam yao mpya ya "Invasion" iuze nakala zaidi ya milioni katika kipindi cha pungufu ya wiki moja.

Katika wimbo huo wa mapenzi, Rick Ross anaanza mwanzo kabisa akisema: "Huh! P- Square Konvict Music, Maybach Music Huh."

Kisha katika sehemu ya 'verse' yake Rick Ross anarap: "Mawazoni mwangu ninachowaza ni yeye tu/ Washa muziki tucheze (bumping ya) P-Square/ Namba moja kwenye gemu na tutabaki hapa/ Huh! daima tunatengeneza ngoma zinazotamba ndani ya Konvict huh!/ Tunazungumzia pesa hapa wewe unazungumza upuuzi...."  

No comments:

Post a Comment