Saturday, June 16, 2012


Chris Brown, Drake wadaiwa kuzipiga

Chris Brown (juu kushoto), Drake (juu kulia) na chini ukumbi uliotokea vurumai baina ya nyota hao wawili
Picha inayoonyesha eneo la kidevu cha Chris Brown lililojeruhiwa katika vurugu hizo


UVUMI umezagaa kwamba Chris Brown na rapa Drake wamezipiga kwenye klabu ya usiku juzi Alhamisi na chanzo kikidaiwa ni Rihanna na kusababisha vurugu kubwa, watu kujeruhiwa na uharibifu mkubwa wa mali za ukumbi wa klabu hiyo ya jijini New York.
Imedaiwa kwamba wawili hao walianza kujibizana kuhusu Rihanna ambaye alikuwa rafiki wa kike wa Chris Brown kabla ya kuachana mwaka 2009 na kuchukuliwa na Drake.
Inasemekana majibizano hayo yalipamba moto na Drake akawa wa kwanza kurusha chupa iliyomkata kidevuni Chris Brown.
Hata hivyo, pande hizo zote mbili zimetoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.
"Chris, Karrueche (mchumba wa Chris) na marafiki zake walikuwa waathirika wa tukio hili baya. Walijeruhiwa sana," alisema msemaji wa Chris Brown, Jeff Raymond. "Chris na watu wake wanatoa ushirikiano wote kwa polisi wa NY wanaochunguza tukio hilo."
Naye msemaji wa Drake, Allison Elbl Striegel, alisisitiza kwamba rapa huyo hakuhusika katika jambo lolote baya ukumbini humo. Alikuwa akiondoka ukumbini wakati vurugu zilipotokea. hakusika na chochote kilichosababisha mtu kujeruhiwa ama uharibifu wa mali."
Upelelezi kuhusu vurugu hizo unaendelea. Na kwa mujibu wa polisi wa New York City, watu nane wake wa waume, wakiwemo ambao hawana hatia walioenda tu klabu kufurahi wamelijeruhiwa kwa kukatwa, kuchubuka na majeraha mengine. Walitibiwa hospitalini na kuruhusiwa. Msemaji wa polisi wa NYPD hakuthibitisha kuhusika kwa Breezy au Drizzy katika vurugu hiyo kubwa.
Ukumbini humo walikuwemo akina Trey Songz, Wale, French Montana na Meek Mill, ambaye aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: "It wasn’t me…. (sauti ya shaggy) lol.”

No comments:

Post a Comment