VIDEO MPYA YA BANANA Ft. DOGO ASLAY YATOKA
Banana Zorro (kulia) akiimba pamoja na baba yake mzazi Zahir Ali Zorro wakati wa moja ya maonyesho ya B-Band. |
Na Ramadhani Mbwaduke
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini na mkurugenzi wa bendi
yake mwenyewe inayokwwenda kwa jina la B-Band, Banana Zahir Zorro, ameachia
video ya wimbo wake mpya wa ‘Nunda’ aliouimba akimshirikisha msanii anayeinukia vyema Dogo Aslay.
Banana ameiambia Blog ya STRAIKA kuwa wimbo huo umerekodiwa
na studio ya Soundcrafters wakati video imefanywa na kampuni inayoaminika kuwa
bora zaidi nchini ya Visual Lab chini ya muongozaji Adam Juma.
“Ni wimbo mzuri sana, nina furaha kwamba mashabiki wangu
wanaweza kupata kitu kipya baada ya kusubiri kwa muda kidogo,” amesema Banana.
Muimbaji huyo anayetamba na nyimbo kama ‘Nzela’, ‘Mama Kumbena’
na ‘Zoba’, amesema mambo wimbo huo mpya na nyingine zake zote zinapatikana
katika maonyesho ya B-Band kila wiki.
B-Band ambayo pia inamjumuisha baba yake mzazi, gwiji wa
muziki nchini Zahir Ali Zorro, inatumbuiza kila Alhamisi hutumbuiza kwenye ukumbi wa Q-Bar
uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, Ijumaa wanapatikana Arabella, Masaki jijini
Dar es Salaam wakati siku ya Jumamosi huitumia kutumbuiza kwenye maeneo
mbalimbali kulingana na mialiko.
No comments:
Post a Comment