Wednesday, June 27, 2012

NASRI AOMBA RADHI KWA KUTUKANA MWANDISHI

Samir Nasri wa Ufaransa akiwaziba mdomo mashabiki wa England baada ya kufunga goli la kusawazisha katika mechi yao ya ufunguzi wa makundi katika fainali za Euro 2012. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1.


PARIS, Ufaransa
KIUNGO wa timu ya taifa ya Ufaransa, Samir Nasri juzi alitoa taarifa ya kuomba msamaha kwa mwandishi wa habari aliyemtukana baada ya timu yake kutolewa katika robo fainali ya Euro 2012 dhidi ya Hispania Jumamosi iliyopita.

"Mambo mengi ambayo hayana ukweli yanazunguka kwa sasa. Napenda mashabiki na watoto kwa ujumla wafahamu kuwa najutia maneno yangu ambayo bila ya shaka yamewashtua," alisema katika ukurasa wake wa Twitter.

Nasri, ambaye aliingia katika kipindi cha pili katika mechi hiyo ambayo Ufaransa walipigwa 2-0 na mabingwa wa Ulaya na dunia Hispania, aliwapita waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri bila ya kusema jambo lolote baada ya mechi.

Alipoulizwa na mwandishi mmoja wa habari atoe maoni yake, alijibu: "Unatafuta matusi, unatafuta matatizo."

Mwandishi huyo alijibu: "Kwenda zako, kama huna cha kusema."

Nasri alimgeukia na kumwambia "fuck you" akifuatia na mfululizo wa matusi, akimtaka mwandishi huyo akutane naye peke yao uso kwa uso.

"Naipenda timu ya Ufaransa, napenda soka na nawaheshimu sana mashabiki. Kwa mengine, ni mambo binafsi baina yangu na baadhi ya waandishi wa habari. Nitafafanua baadaye," Nasri aliongeza.

---------

No comments:

Post a Comment