Saturday, June 16, 2012

BALOTELLI AMCHEFUA KOCHA ITALIA




Mario Balotelli wa Italia akienda benchi wakati wa mechi yao ya Kundi C la UEFA Euro 2012 dhidi ya Croatia kwenye Uwanja wa The Municipal Alhamisi Juni 14, 2012 mjini Poznan, Poland.



Mario Balotelli wa Italia akipumzishwa wakati wa mechi yao ya Kundi C la UEFA Euro 2012 dhidi ya Croatia kwenye Uwanja wa The Municipal Alhamisi Juni 14, 2012 mjini Poznan, Poland.


Mario Balotelli "akifungishwa tela" na Luka Modric wa Croatia wakati wa mechi yao ya Kundi C la UEFA Euro 2012 dhidi ya Croatia kwenye Uwanja wa The Municipal Alhamisi Juni 14, 2012 mjini Poznan, Poland.


KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli alikasirishwa mno na mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli wakati wa sare yao ya 1-1 dhidi ya Croatia.
Prandelli amebainisha kwamba alitumia muda mwingi kumpigia makelele bila ya mafanikio kabla ya kuamua kumtoa mshambuliaji huyo katika sare hiyo ya Euro Alhamisi.
Prandelli alisema: "(Sababu ya) kumtoa Mario? Nilikaukiwa sauti yangu kwa kumpigia kelele kwa dakika 15 na sikufanikiwa kumrekebisha alivyokuwa akijipanga uwanjani katika uchezaji wake.
"Kama tunampenda kijana huyu, ni lazima tumweleze mambo haya, tumweleze ukweli.
"Je, ana uchungu na jezi ya timu ya taifa ya Italia? Kama unataka kuwa mchezaji gwiji, unapaswa kutambua kwamba utakumbana vikwazo.
"Alikuwa akirudi nyuma sana lakini alikuwa hapati mpira. Unaporudi nyuma sana unatakiwa upate mpira au vinginevyo uwe mbele kabisa katika nusu yao."
Aliongeza: "Sitamzuia kucheza mechi nyingine lakini hakuna mtu anapaswa kusema 'mimi ndio mimi' ndani ya kikosi chetu. 
"Mnaniuliza ni kwa muda mrefu kiasi gani Italia inahitaji kusubiri Balotelli atusaidie? Siku tatu. Tunatarajia majibu ya vitendo kutoka kwake.”

No comments:

Post a Comment