Monday, June 18, 2012


DIAMOND KUNG'ARISHA MISS VYUO VIKUU DAR


Na Mwandishi Wetu
NYOTA Bongofleva, Naseeb Abdul a.k.a. Diamond Platnumz anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka mrembo wa Miss Dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond, onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.

Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam

"Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania," alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT) ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yolla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Spoti Kizaazaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.


No comments:

Post a Comment