Saturday, July 6, 2013

NEYMAR, JORDI ALBA WAPASULIWA MAKOO

Neymar wa Brazil akiwaburuza wachezaji wa Hispania, Jordi Alba (kushoto), Sergio Ramos na Cesar Azpilicueta (kulia) wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Mabingwa wa Mabara 2013 kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil Juni 30, 2013.
Neymar (kushoto) wa Brazil akishangilia goli lake baada ya kumtungua kipa wa Hispania Iker Casillas (aliyelala chini) huku beki Alvaro Arbeloa (kulia) akijiuliza wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Mabingwa wa Mabara 2013 kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil Juni 30, 2013.

Mimi Barca mwenzako unanichapa kiatu....! Neymar akigaagaa chini baada ya kuchapwa kiatu na beki wa Hispania Gerard Pique ambaye alikula nyekundu kwa kumzuia nyota huyo asiende kufunga wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Mabingwa wa Mabara 2013 kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil Juni 30, 2013. .
Japo mmetufunga sisi ni Barca..... Xavi wa timu ya taifa ya Hispania akimpongeza Neymar wa Brazil baada ya mechi yao ya fainali ya Kombe la Mabingwa wa Mabara 2013 kwenye Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil Juni 30, 2013.


NYOTA wa Barcelona, Neymar na Jordi Alba wamefanyiwa kimafanikio upasuaji mdogo wa koo kwa ajili ya kuondoa tonsils jana, klabu hiyo ya Catalunya imethibitisha.

Upasuaji huo ulipangwa na Barca kwa matumaini ya kumaliza tatizo hilo linalojirudia baina ya wawili hao.

Klabu hiyo ilisema upasuaji ulienda vyema kama ulivyopangwa na kubainisha kwamba watakuwa nje ya mchezo kwa siku chache sana.

"Ijumaa hii, Neymar na Jordi Alba wamefanyiwa kimafanikio upasuaji wa matatizo yao ya 'tonsillitis', ambayo yalikuwa yakijirudia katika wiki za karibuni," klabu ilibainisha katika tovuti yake.

"Muda wa kupona kwa wachezaji wote wawili ni kati ya siku 10."

Wachezaji hao walilazimika kusubiri hadi kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mabingwa wa Mabara - ambalo timu ya Neymar ya Brazil iliifunga ya Jordi Alba ya Hispania 3-0 katika fainali - kabla ya kwenda kufanyiwa upasuaji huo.

No comments:

Post a Comment