Sunday, June 16, 2013

MARIETA ASHINDA REDD'S MISS CHANG'OMBE


Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati, Happiness Watimanywa (katikati) akiwa na uso wa furaha mara baada ya kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma. Kushoto ni mshindio wa pili Sabrina Juma kutoka mkoani Tabora na kulia ni mshindi wa tatu Jackline.

MREMBO Marieta Boniface juzi usiku alitwaa taji la Redd’s Miss Chang’ombe 2013 katika kinyang’anyiro kikali kilichofanyika kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Marieta aliwashinda warembo wengine 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Kutokana na ushindi huo, Marieta alizawadiwa pikipiki yenye thamani ya Sh. milioni 1.5 ambayo ilitolewa na wadhamini wenza Kampuni ya Kishen Enterprises Ltd.

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi ndiye aliyemkabidhi zawadi hiyo na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na shindano hilo na yupo tayari kulisaidia zaidi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa taji, Marieta alisema anaamini kwa dhati atafanikiwa kufika mbali zaidi kwani amedhamiria kuhakikisha anaibeba Chang’ombe katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Post a Comment