Wachezaji wa Simba (juu) na wa Yanga (chini) wakishangilia katika mechi zao tofauti za Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu. Nani atacheka Jumamos hiii? |
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu (2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14 kupambana katika viwanja saba tofauti.
Mechi zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom toleo la 2012.
Yanga ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa Mbeya.
Mgambo Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka Kilimanjaro).
Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).
Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni Josephat Magazi wa Singida.
No comments:
Post a Comment