Saturday, April 20, 2013

LIONEL MESSI SASA YUKO 'FITI' KINOMA... YUMO KATIKA WAKALI WANAOSAKA USHINDI WA MECHI TATU TU ILI BARCA WATANGZWE RASMI KUWA MABINGWA WA LA LIGA KABLA KUMALIZIKA MSIMU

Messi akijifua na wenzake jana. Anayetabasamu kushoto ni David Villa.
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amepona kabisa msuli wa paja na sasa yuko 'fiti' kuungana na wenzake katika kusaka ushindi wa mechi tatu za La Liga, Ligi Kuu ya Hispania ili watangazwe kuwa mabingwa rasmi kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2012/2013.

Wakipata pointi tisa kuanzia leo Jumamosi (April 20, 2013) watakapovaana na Levante, Barca watajihakikishia taji la La Liga ambalo hivi sasa linashikiliwa na mahasimu wao wa jadi, Real Madrid.

Mechi nyingine za Barca katika La Liga baada ya kuwavaa Levante leo ni dhidi yaAthletic de Bilbao na Real Betis.

Wakati huohuo, Barça wana kibarua cha kujiweka 'fiti' pia kabla ya kuwavaa Bayern Munich katika mechi yao ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa Jumanne mjini Munich, Ujerumani.

No comments:

Post a Comment