Monday, April 1, 2013

GOLI KALI LA BA LAING'OA MAN UNITED KOMBE LA FA

Demba Ba akishangilia bao lake
Hoii... Wachezaji wa Manchester United wakiwa hoi huku wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Demba Ba baada ya kufunga goli
Ba akishangilia goli lake huku akifuatwa na Hazard na Oscar
Safari hiyo.... Demba Ba akimpa upaja Smalling
Chukua hiyo... Chicharito akitoa pasi 
Tulia wewe... Evra akimpita Oscar
Ba akishangilia goli lake pamoja na mashabiki wa Chelsea

Mata (kulia) akipiga shuti nje dhidi ya beki Chris Smalling na kipa De Gea
Gooooooooo! Mnyama Demba Ba akitupia kitu mbele ya Rio Ferdinand na Smalling. Huyu jamaa anamtesaga sana Rio.

LONDON, England
GOLI kali lililofungwa na Demba Ba liliwapa Chelsea ushindi wa 1-0 ulioiengua Manchester United katika robo fainali ya Kombe la FA katika mechi yao ya marudiano kwenye Uwanja wa Stamford Bridge leo, na kuwafanya mabingwa hao watetezi kutinga nusu fainali ambapo watapambana na Manchester City.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal, ambaye alikuwa ameifungia Chelsea goli moja tu katika mechi 10 zilizopita, alifunga goli lake leo katika dakika ya 49 wakati alipouacha mpira wa pasi ndefu ya Juan Mata upite juu ya bega lake kabla ya kujinyoosha na kufunga kwenye kona ya mbali iliyomfanya kipa David De Gea abaki amepigiliwa misumari.

Kipa wa Chelsea, Petr Cech aliokoa kifundi dakika 14 baadaye kufuatia mpira wa kichwa uliopigwa na Javier Hernandez na mpira kupaa juu kidogo ya lango.

Chelsea, ambao wametwaa kombe hilo mara nne katika misimu sita iliyopita, watacheza dhidi ya Man City, mabingwa wa mwaka 2011, kwenye Uwanja wa Wembley Aprili 14.

Klabu ya Ligi daraja la Kwanza ya Millwall itacheza dhidi ya Wigan Athletic katika mechi nyingine ya nusu fainali Wembley siku moja kabla.

No comments:

Post a Comment