Saturday, March 16, 2013

WENGER NI "MPUUZI", ASEMA MANCINI

Roberto Mancini - Man City
Arsene Wenger - Arsenal

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amemuita kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuwa ni "stupid" kufuatia madai yake aliyoyatoa kuhusu Ligi ya Klabu Bingwa.

Kufuatia kutolewa kwa Arsenal na Bayern Munich Jumatano usiku, Wenger alidai kwamba kilichotokea ni "onyo kubwa" kwa Ligi Kuu ya England kutokana na kiwango kibovu cha timu zake barani humo msimu huu.

Lakini Mancini alisema: "Mwaka jana Chelsea walitwaa ubingwa wa Ulaya na mwaka huu ligi ya England ilikuwa na timu tatu kwenye robo fainali ya Ligi ya Europa.

"Kwa miaka mitatu ama minne timu za England zimetwaa ubingwa wa Ulaya, au zimetinga fainali. Kwa mwaka mmoja, timu nyingine zimefanikiwa.

"Niliposoma jambo hili kuhusu soka la Uingereza kwamba liko chini niliona ni upuuzi.

"Haiwezekani kutwaa ubingwa kila mwaka. Kauli hizi ni kama za Italia ambako ukishinda mechi moja tu wewe ndiye bora "kuliko" na ukifungwa moja hiyo ni kashfa.

"Hili ni soka. Kama kila mwaka timu hiyo hiyo inashinda, soka lingekuwa kitu kingine.

"Soka ni zuri kwa sababu hii. Kila mwaka mambo yanaweza kubadilika."

No comments:

Post a Comment