Tuesday, March 19, 2013

WENGER AJITOSA KUMNG'OA ALEXIS SANCHEZ WA BARCA... ACHUANA VIKALI NA INTER MILAN WALIO TAYARI KUMTWAA KWA "HELA NDEFU"

Alexis Sanchez
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amevutiwa na mshambuliaji Alexis Sanches wa klabu ya Barcelona na tayari ameanza mazungumzo ya kumsajili nyota huyo, imefahamika leo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile ameonekana "kufulia" uwanjani msimu huu na hivyo kuhusishwa na uhamisho utakaomuondoa Barca.

Gazeti la AS limesema leo kuwa Wenger amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na wakala wa Sanchez kwa nia ya kumshawishi ili amjumuishe katika kikosi chake.

Hata hivyo, rais wa Inter Milan ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia, Massimo Moratti, amekutana pia wiki iliyopita na wakala wa mchezaji huyo nyota wa zamani wa Udinese kwa nia ya kumtwaa kwa usajili utakaowagharimu mabilioni ya pesa.

No comments:

Post a Comment