Monday, March 11, 2013

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA MZEE YUSUF MZIMBA ALIYELAZWA MUHIMBILI KWA KUGONGWA NA BODABODA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole mzee Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee maarufu wa klabu ya Dar es Salaam, Young Africans (YANGA) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia apate nafuu ya haraka. Picha: IKULU

No comments:

Post a Comment