Wednesday, February 6, 2013

SAMATTA NOMAAA, AWAZIMA CAMEROON TAIFA

Kipa wa 'Indomitable Lions'ya Cameroon, Effala Komguep akiokoa hatari langoni mwake wakati wa mechi yao dhidi ya Taifa Stars ya Stars ya Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Stars ilishinda 1-0.  

STRAIKA klabu ya TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta alikuwa shujaa leo baada ya kufunga goli pekee lililowapa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika, Cameroon katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Samatta aliifungia Stars goli hilo lililoamua mechi dakika moja kabla ya mchezo kumalizika akiunganisha kiufundi krosi safi ya kiungo wa Yanga, Frank Domayo kutokea wingi ya kulia.

Wenyeji wangeweza kupata ushindi mnono zaidi kama penalti ya beki Erasto Nyoni katika dakika ya 28 isingepanguliwa na kipa wa Cameroon, Effala Komguep.

Cameroon iliyomkosa nahodha wake Samuel Eto'o wa klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi na kiungo Alex Song wa Barcelona ya Hispania, ambao ni majeruhi, ilijikuta ikiadhibiwa penalti hiyo ya mapema katika baada ya beki wao wa kati, Ngoula Patrick, kushika mpira wakati akijaribu kuokoa hatari langoni mwao.

Hata hivyo, penalti hiyo iliyotolewa na refa Munyemana Hudu ilipanguliwa na kipa Patrick kabla ya mabeki wa Cameroon kuosha mpira na kuwa kona butu kwa Stars.

Ushindi huo unaifanya Stars ijivunie matokeo yake ya karibuni baada yaDesemba 22 mwaka jana kuwabwaga mabingwa wa Afrika, Zambia 'Chipolopolo', kwa goli 1-0 la Mrisho Ngassa kwenye uwanja huo huo.

Vikosi vilikuwa; Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomarui Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar 'Sure Boy', Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto/ Thomas Ulimwengu (dk. 56) na Amri Kiemba.

Cameroon: Effala Komguep, Bonnoit Assou-Ekotto, Aminou Bouba, Mgoula Patrick, Nyom Allan, Pierre Wome, Kingue Mpondo, Bedimo Henri/ Ashu Clovis (dk.73), Tchami Herve/ Elundu (dk.57), Olinga Fabrice/ Makoun Thierri (dk. 68) na Aboubakar Vincent/ Bakinde Gerrard (dk. 85).   

1 comment:

  1. kiukweli jana tuliona gemu ya kwenye kitabu. loooooooooooooo NYOTA imemwona kipofu

    ReplyDelete