Ronaldo (kulia) na Luka Modric wakishangilia baada ya Ronaldo kufunga goli jingine dhidi ya Sevilla. |
Goooooh...! Ronaldo (kulia) akifunga goli dhidi ya Sevilla licha ya kuchungwa vikali na Federico Fazio wa Sevilla (kushoto). |
Karim Benzema wa Real akizongwa na mabeki watatu wa Sevilla. |
|
Mzuka umepanda...! Arjen Robben wa Bayern Munich akiruka uzio ili wakati akiwapa mashabiki jezi yake kufuatia furaha ya ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Schalke 04 wakati wa mechi yao ya Bundesliga mjini Munich, Ujerumani leo Feb. 9, 2013. (Picha: Reuters) |
Sijui nilie....! Kocha Roberto Mancini wa Manchester City akitazama saa yake wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southamtpon kwenye Uwanja wa St Mary, leo Feb 9, 2013. Man City ilipata kipigo cha 3-1. (Picha: Reuters) |
Tunatishaaaa...! Wachezaji wa Southampton wakishangilia ushindi dhidi ya mabingwa, Man City baada ya kumalizika kwa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Februari 9, 2013. )Picha: Reuters) |
Straika wa Napoli, Edinson Cavani (kushoto) akimtoka beki wa Lazio, Giuseppe Biava wakati wa mechi yao ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia kwenye Uwanja wa Rome, leo Feb. 9, 2013. (Picha: Reuters) |
Kachinje jogoo...! Kipa wa Schalke, Timo Hildebrand (kulia) akiishika mlingoti wa goli baada ya kuokoa shuti la straika wa Bayern Munich, Arjen Robben wakati wa mechi yao ya Bundesliga, Ligi Kuu ya Ujerumani leo Februari 9, 2013. Bayern walishinda 4-0. (Picha: Reuters) |
Inakuwaje? Straika Edinson Cavani wa Napoli akisikitika baada ya kukosa goli wakati wa mechi yao ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia dhidi ya Lazio kwenye Uwanja wa Olympic mjini Rome, leo Februari 9, 2013. (Picha: Reuters) |
Cristiano Ronaldo ametupia magoli matatu peke yake na kutengeneza jingine moja lililowekwa wavuni na Karim Benzema wakati Mreno huyo alipopiga hat-trick yake ya 17 katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kuisaidia Real Madrid kuibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Sevilla kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu usiku huu (Jumamosi Februari 9, 2012).
Magoli hayo yamemfanya Ronaldo awe kinara wa orodha ya wakali waliowahi kupiga hat-trick katika misimu 10 iliyopita ya La Liga, akifuatiwa na Lionel Messi aliyefikisha hat-trick 16 na ambaye saa chache zijazo (Jumapili mchana, Februari 10, 2013) atakuwa na nafasi ya kumfikia Ronaldo wakati klabu yake ya Barcelona itakapowakaribisha Getafe kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Ronaldo pia ameendelea kujiwekea rekodi nzuri ya mabao tangu atue Real Madrid baada ya kufikisha magoli 182 katikia mechi 179 alizoichezea timu hiyo iliyopoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao wa La Liga msimu huu. Straika huyo amefikisha magoli 24 katika mechi 22 za La Liga msimu huu, huku akifikisha magoli 36 katika mechi 35 za michuano yote msimu huu. Kabla hata ya kuwavaa Getafe, Messi anaongoza orodha ya wafungaji katika La Liga baada ya kufikisha magoli 33.
Goli alilofunga Benzema aliyetumia vyema pasi ya Ronaldo lilikuwa ni la 50 katika La Liga kwa straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa tangu aanze kuichezea Real Madrid.
Manu ndiye aliyefungia Sevilla bao la kufutia machozi wakati timu hiyo ikipata kipigo cha nane katika mechi zao tisa zilizopita dhidi ya Real Madrid.
MATOKEO MECHI NYINGINE LA LIGA
Katika mechi nyingine za La Liga zilizochezwa leo, matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mallorca 1 - 1 Osasuna
Celta 0 - 1 Valencia
Levante 1 - 2 Malaga
Deportivo 0 - 3 Murcia
MATOKEO LIGI KUU ENGLAND
Tottenham 2 - 1 Newcastle
Chelsea 4 - 1 Wigan Athletic
Norwich 0 - 0 Fulham
Stoke 2 - 1 Reading
Sunderland 0 - 1 Arsenal
Swansea 4 - 1 QPR
Southampton 3 - 1 Man City
MATOKEO SERIE A, LIGI KUU YA ITALIA
Juventus 2 - 0 Fiorentina
Lazio 1 - 1 Napoli
MATOKEO BUNDESLIGA, LIGI KUU YA UJERUMANI
Hannover 1 - 0 Hoffenheim
Dortmund 1 - 4 Hamburger
M'bach 3 - 3 Leverkusen
Greuther 0 - 1 Wolfsburg
Stuttgart 1 - 4 Bremen
Eintracht 0 - 0 Nürnberg
Bayern 4 - 0 Schalke
MATOKEO LIGUE 1, LIGI KUU YA UFARANSA
PSG 3 - 1 SC Bastia
Etienne 4 - 1 Montpellier
Ajaccio 1 - 0 Bordeaux
Nancy 1 - 2 Reims
Troyes 0 - 0 Sochaux
Nice 1 - 1 Lorient
Valenciennes 2 - 1 Brestois
No comments:
Post a Comment