Monday, February 18, 2013

PAUL INCE ATANGAZWA KOCHA MPYA WA TIMU YA MWANAE TOM YA BLACKPOOL

Paul Ince na mwanae, Tom, wakihudhuria tuzo za MOBO 2012 kwenye Ukumbi wa Echo Arena mjini Liverpool, England Novemba 3, 2012.

MCHEZAJI wa kimataifa wa zamani wa England, Paul Ince amerejea kwenye kazi yake ya ukocha baada kukabidhiwa mikoba ya kuifundisha klabu ya daraja la pili ya Blackpool, ambako mwanaye Tom ni mfungaji anayeongoza.

Ince (45), ambaye alijenga jina lake katika kiungo cha Manchester United kabla ya kuhamia Inter Milan na Liverpool, amekuwa nje ya ajira tangu alipoondoka katika klabu ya daraja la chini ya Notts County mwaka 2011.

"Kwa kuzingatia kwamba nimekuwa nikiishuhudia klabu hii ikicheza kwa miezi 14 iliyopita, ni jambo la kushangaza kwamba kukaa hapa kama kocha, baada ya kuiangalia Blackpool kama shabiki pamoja na kumuangalia mwanangu akicheza," Ince, ambaye aliifundisha kwa muda mfupi Blackburn Rovers ya Ligi Kuu ya England mwaka 2008, alisema katika taarifa ya klabu hiyo jana.

No comments:

Post a Comment