Wednesday, February 27, 2013

ONA MBINU KALI ALIYOTUMIA JOSE MOURINHO KWA MABEKI WAKE LEO KUHUSU NAMNA YA 'KUMFUNIKA' LIONEL MESSI KATIKA MECHI NZIMA YA KOMBE LA MFALME WALIYOSHINDA 3-1 BILA HATA KUMCHEZEA MIRAFU AMBAYO SIKU ZA NYUMA ILIKUWA IKIWAPA KADI ZA NJANO NA HATA NYEKUNDU... NJIA HII INAITWA 'TUNDU' KAMA LA NDEGE... NDIYO HIYO PIA WALIYOITUMIA MILAN WAKATI WAKIIPIGA BARCELONA 2-0

Leo huendi kokote...! Essien Ikulia) akimdbiti Lionel Messi wa Barca  

Tulia hukooo...! 

MADRID, Hispania
Mbinu ya kocha José Mourinho katika kuhakikisha kuwa mabeki wake 'wanamfunika' Lionel Messi na kuhakikisha kuwa haleti madhara katika muda wote wa mechi na huku pia wakiepuka kulimwa kadi kwa sababu yake imetajwa kuwa ni ile ya kutumia mfumo uitwao "Tundu" (the cage)

Mbinu hiyo pia ndiyo iliyotumiwa katika mechi yao ya kwanza ya 'el clasico' ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme kenye Uwanja wa Santiago Bernabu ambapo matokeo yalikuwa 1-1.

Na katika mechi ya marudiano ya Kombe la Mfalme iliyomalizika usiku huu na Real kuibuka kidedea kwa kuitandika Barca mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Camp Nou kwa mabao 3-1, mbinu ya mfumo wa "tundu" ndiyo iliyotumika pia kumpoteza kabisa Messi ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia.

Mourinho alifurahia sana vijana wake walivyoielewa mbinu hiyo na kuonekana akiwapongeza katika mechi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Bernabéu, ikiwa ni mara tu baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa.

Kimsingi, mfumo huu wa 'tundu' unawataka mabeki kutomruhusu Messi apokee mpira na kwamba, wakati atakapofanya nhivyo, ni lazima anyimwe muda wa kufikiri juu ya nini cha kufanya.

Mbinu hii ya 'tundu' ndiyo iliyotumiwa na kocha wa Milan, Massimiliano Allegri, ambaye aliwaagiza Mexes, Zapata, Abate, Ambrosini na Constant kumzunguka Messi na kumvamia kila mara anapopokea pasi kutoka kwa wenzake.
Milan iliwalipa mno mbinu hii kwani katika dakika zote tisini za mechi yao ya kwanza ya hatua ya 16-bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Messi hakupata nafasi ya kupiga shuti lo9lote lililolenga goli katika dakika zote tisini, licha ya kwamba timu yake ilimiliki mpira kwa asilimia 65 na kucheza pasi zilizofika zaidi ya 650, huku Milan wakipeana pasi sahihi 261. Timu nzima ya Barca ilijikuta pia ikiathiriwa na mbinu ya 'the cage' kwani katika dakika zote tisini, walifanikiwa kupiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango kulinganisha na sita ya Milan, mawili yakitinga wavuni na kuwapa ushindi Waitaliano.

Na leo tena, Messi alichungwa kwa staili hiyohiyo ya 'the cage' na kujikuta akishindwa kufurukuta mbele ya mabeki ngangari wa Real Madrid walioiva kwa mbinu hiyo na hadi mwisho, Barca walipiga mashuti machache mno yaliyolenga lango wakati wakichapwa 3-1; huku Cristiano Ronaldo akitupia mabao mawili na jingine likifungwa na Raphael Varane. La kujifutia machozi la Barca limefungwa na Jordi Alba.

No comments:

Post a Comment