Wednesday, February 13, 2013

MOURINHO: BAADA YA REAL NARUDI ENGLAND

Jose Mourinho

JOSE Mourinho amesisitiza kwamba ajira yake itakayofuata baada ya Real Madrid itakuwa ni kufundisha soka katika Ligi Kuu ya England.

Hatma ya Mourinho Bernabeu imekuwa katika hatihati kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya Real kwenye mbio za kutetea taji lao la Ligi Kuu ya Hispania huku wakijiandaa kuikabili Manchester United katika mechi ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya leo.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 50, ame,kuwa akihusishwa na mipango ya kutua Man United, Manchester City na Chelsea.

Alipoulizwa ni lini anatarajia kurejea England, kocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema: "Baada ya Real. Napenda kila kitu (kuhusu Ligi Kuu ya England).

Aliongeza: "Hakika itakuwa ndiyo hatua yangu inayofuata."

Mourinho pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Paris St-Germain - lakini ameweka wazi kwamba anaona hatma yake ni kurejea haraka England.

No comments:

Post a Comment