Wednesday, February 20, 2013

MATOKEO MABOVU' KIDATO CHA NNE YAZUA MAAFA ... MADENTI WAJIPIGA VITANZI HADI KUFA MKOANI TABORA NA DAR KISA KUPATA 'DIVISHENI ZIRO' NA "DIVISHENI FOUR"... POLISI WASEMA MIILI IMEKUTWA VYUMBANI, STOO...!

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Joyce Ndalichako
Matokeo mabovu kuliko yote ya kidato cha nne kuwahi kutokea katika historia ya taifa la Tanzania yamezua balaa la aina yake baada ya wanafunzi wawili kujiua kwa kujipiga vitanzi hadi kufa.

Taarifa zilizothibitishwa leo na jeshi la polisi zimeeleza kuwa madenti waliojiua kutokana na matokeo hayo ni wa jijini Dar es Salaam na mwingine kutoka mkoa wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,  Anthony Rutta, amesema leo kuwa mhitimu aliyejiua mkoani humo ni  Michael Fidelis (19) mkazi wa Mtaa wa Mwinyi, Kata ya Chemchem aliyemaliza katika Shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora.

Kamanda Rutta amesema kuwa Fidelis amejiua kwa kujinyonga hadi kufa baada ya kwenda kuangalia matokeo juzi Jumatatu (Februari 18, 2012), saa 11:00  jioni. Baadaye akakutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila, kisa ikiwa ni kupada divisheni ziro.

Sehemu ya ujumbe alioacha marehemu Fidelis ulisomeka hivi: "Nisamehe sana mama, usitafute mchawi... nakupenda sana. Uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo mabaya, nakutakia maisha mema.”

Matokeo ya shule ya Kanyenye yanaonyesha kuwa wahitimu 85 walipata sifuri na hakuna aliyefaulu kwa daraja la kwanza wala la pili.

Jijini Dar es Salaam, aliyejiua kwa kujipiga kitanzi baada ya kufeli ni aliyekuwa denti wa Shule ya Sekondari Debrabant iliyopo Mbagala, wilayani Temeke, Barnabas Venant (18).

Kamanda wa Engelbert Kiondo wa mkoa wa kipolisi Temeke, amesema leo kuwa Vicent alikuwa akiishi Nzasa na amejinyonga kwa manila akiwa ndani ya stoo ya nyumba yao juzi saa 10:00 jioni baada ya kuambulia divisheni 'four', kinyume kabisa na matarajio yake.

Katika matokeo yaliyotangazwa juzi, asilimia 60 ya wanafunzi wote wamefeli kwa kupata "divisheni ziro" na jumla yao, ukichanganya na wale waliopata "divisheni four" ni asilimia zaidi ya 94; idadi ya kubwa zaidi ya kufeli kuwahi kutokea katika taifa hili.


  

1 comment:

  1. DAMU ZA WATOTO WETU NAZIWE JUU YA HAO WALIOFANYA UBATILI KATIKA MATOKEO HAYO KWANI HATAACHA KUJIBU KILIO CHA MASIKINI SISI TUSIOWEZA KUPELEKA WATOTA ZA BINAFSI EE MUNGU BABA YETU UWAREHEMU WATOTO WETU KWANI HAYO NI MATOKEO YA UONGOZI USIO NA MAPENDO WALA HURUMA NA WAKUMDHALILISHA MLALA HOI JAPO UKIKOSA ADA MZAZI UNAFUNGULIWA MASHITAKA HUKU ELIMU YA KUBURUZAAAAAAAAAAAAA!

    ReplyDelete