Saturday, February 23, 2013

LIONEL MESSI: MILAN WATATUKOMA CAMP NOU

Duh... leo ngoma nzito! Lionel Messi (aliyeinama) wakitafakari na Xavi baada ya kupigwa goli la pili wakati wa mechi yao dhidi ya AC Milan Jumatano.
Baada ya mechi kumalizika
BARCELONA, Hispania
Lionel Messi wa Barcelona ametoa kauli yake ya kwanza baada ya kipigo kinachouma cha mabao 2-0 walichokipata Jumatano kutoka kwa AC Milan katika mechi yao ya kwanza ya ugenini ya hatua ya 16-bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kusema kuwa wapinzani wao walicheza vizuri zaidi na kustahili kushinda, lakini watambue kuwa watakiona chamoto katika mechi yao ya marudiano itakayopigwa Machi 12 kwenye Uwanja wa Nou Camp.

"Hatukucheza vizuri, lakini sisi wenyewe tunajiamini kwamba tunao uwezo wa kulipiza kisasi. Naamini tunaweza kubadili matokeo," amesema Messi.

Maneno haya ya mshindi mara nne mfululizo wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia yametolewa pia kupitia mtandao wa kijmii wa China.

Katika mechi hiyo ya Jumatano, Barca waliomiliki mpira kwa asilimia 65, walishindwa kabisa kufurukuta ambapo katika dakika zote 90, waliishia kupiga mashuti mawili tu yaliyolenga goli na Messi aliyebanwa mwanzo - mwisho alishindwa kupiga walau shuti moja tu la kulenga goli. Milan walipiga mashuti 6 ya kulenga goli na mawili yakatinga wavuni, yakipigwa na Waghana Kevin - Prince Boateng na Sulley Muntari.

No comments:

Post a Comment