Monday, February 4, 2013

ETO'O, KASEJA KULONGA NA WAANDISHI

Eto'o (kushoto) na Alex Song

Makocha wa timu za Tanzania, Kim Pousen na Cameroon, Jean Paul Akono na manahodha wao Juma Kaseja Juma na Samuel Eto'o Fils kesho (Februari 5 mwaka huu) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia pambano la keshokutwa.

Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo, mkutano huo na waandishi wa habari ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa itakayofanyika Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars ambayo iko kambini, ilianza mazoezi yake leo saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa wakati Cameroon itajifua uwanjani hapo kesho Jumanne.

No comments:

Post a Comment