Kombe tusubiri mwaka wa tisa... Jack Wilshere wa Arsenal akijiuliza baada ya timu yake kufungwa 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Februari 16, 2013. |
Francis Coquelin wa Arsenal akijiuliza baada ya timu yake kufungwa 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Februari 16, 2013. |
Dah hawa jamaa ndo wametutoa! |
Ningekuwa Chelsea nshafukuzwa ila jamaa nawapenda kwa uvumilivu... Kocha wa Arsenal akiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Blackburn |
GOLI la dakika za lala salama kutoka kwa Colin Kazim-Richards liliishangaza Arsenal wakati Blackburn Rovers ilipotinga robo fainali ya Kombe la FA.
Arsenal walitawala huku Gervinho akishindwa kulenga lango kutokea katika nafasi nzuri na kipa Jake Kean aliokoa mashuti kadhaa kiufundi.
Tomas Rosicky aligongesha besela baada ya mapumziko lakini timu hiyo ya ligi daraja la kwanza ilipata goli wakati Kazim-Richards alipomalizia shuti lililotemwa la Martin Olsson.
Theo Walcott alibaniwa goli katika dakika za lala salama wakati matumaini ya Arsenal ya kumaliza ukame wa miaka nane wa makombe yakipata pigo.
Hiyo inamanisha kwamba timu Arsene Wenger imebakisha ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tu kama wanahitaji kutwaa taji msimu huu, kwani tayari walishatolewa kwenye Kombe la Capital One na timu ya Daraja la Tatu ya Bradford Desemba.
Matokeo ya mechi za Jumamosi Feb 16, 2013 za Kombe la FA:
No comments:
Post a Comment