Thursday, January 10, 2013

WALCOTT ANASTAHILI NUSU TU YA OFA MPYA ALIYOPEWA, ADAI NYOTA WA ZAMANI ARSENAL

Theo Walcott

KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Stewart Robson ameponda ofa ya mkataba mpya aliyopewa Theo Walcott.

Walcott anajiandaa kusaini mkataba mpya utakaompatia mshahara wa paundi 88,000 kwa wiki.

"Kama Olivier Giroud na Lukas Podolski wanacheza vyema na Santi Cazorla anafunga magoli, Theo Walcott angeachwa tu aondoke Arsenal Januari,” Robson aliiambia talkSPORT.

“Suala la Walcott limekuja katika kipindi sahihi tu na matokeo yake atalipwa mara mbili ya anachostahili.

“Theo Walcott anapewa sifa ambazo hana. Ni mzuri kwenye kasi na anaonekana kama mmaliziaji mzuri lakini uchezaji wake kwa ujumla si mzuri sana. Wachezaji wengine wengi Arsenal wana ufundi wa kusoma mchezo kuliko yeye.

“Nilitamani pesa hizo zingetumika kuwabakisha Robin Van Persie, Cesc Fabregas Samir Nasri, Alex Song na Gael Clichy na wachezaji wote walioondoka kabla ambao walikuwa wa viwango vya juu.

“Walcott ni 'homa ya vipindi'. Anaweza kucheza vizuri katika mechi kadhaa kisha anapotea kama alivyofanya dhidi ya Southampton ambapo alishindwa hata kukaa na mpira. Alilazimika kupelekwa kwenye wingi ya kulia kwa sababu alikuwa hana mchango katikati."

No comments:

Post a Comment