Thursday, January 10, 2013

MJADALA WA LIGI BORA NI IPI... MASHABIKI WATAKA MECHI IPIGWE NYOTA WA LA LIGA vs NYOTA WA LIGI KUU YA ENGLAND

Kikosi Bora cha Ligi ya England (kushoto) dhidi ya kikosi cha La Liga (kulia)

BAADA ya kutangazwa kwamba wachezaji wote 11 wa kikosi cha FIFA 2012 wanatokea katika Ligi Kuu ya Hispania, kumekuwa na malalamiko kutoka England ambao wamependekeza ipigwe mechi baina ya wachezaji bora wa La Liga dhidi ya bora wa Ligi Kuu ya England.

Jopo la waandishi wa habari wa Uingereza limeteua majina ambayo linaamini kuwa ndiyo bora kabisa katika Ligi Kuu ya England ambao wametajwa kuwa ni Joe Hart, Pablo Zabaleta, Vertonghen, Vincent Kompany, Leighton Baines, Marouane Fellaini, David Silva, Yaya Toure, Gareth Bale, Sergio Aguero na Robin van Persie.

Kikosi hicho kimetakiwa kupambana na kikosi cha La Liga ambacho kimetajwa kuwa ndicho kikosi bora duniani.

Kikosi cha La Liga kinaundwa na Iker Casillas, Dani Alves, Marcelo, Sergio Ramos, Gerard Pique, Xabi Alonso, Xavi Hernandez, Andres Iniesta, Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao na Lione Messi.

Lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao mmoja wa nchini Hispania kupitia swali lililosema: "Nani atashinda mechi baina ya nyota wa La Liga na Ligi Kuu ya England?" wasomaji hao wamesema wachezaji wa Ligi Kuu ya Hispania watawashambaratisha vibaya wachezaji wa Ligi Kuu ya England.

Zaidi ya kura asilimia 91 zilizema kwamba nyota wa La Liga watashinda kwa ushindi mnono wakati asilimia 9 walisema nyota wa Ligi Kuu ya England watashinda.

Zaidi ya watu 81,000 walipiga kura katika utafiti huo.

No comments:

Post a Comment