Monday, January 7, 2013

TEVEZ: NAJARIBU KUMSAIDIA BALOTELLI

Mario Balotelli akitafakari wakati timu yake ikijiandaa kucheza dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Etihad juzi Jumamosi
Kocha wa Watford, Muitalia Gianfranco Zola akizungumza na Muitalia mwenzake Mario Balotelli wa Manchester City baada ya firimbi ya mwisho wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England juzi Jumamosi Januari 5, 2013. Man City ilishinda 3-0.
Sikia kijana wewe 'unajua' kinoma ila.... Kocha wa Watford, Muitalia Gianfranco Zola akizungumza na Muitalia mwenzake Mario Balotelli wa Manchester City baada ya firimbi ya mwisho wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England juzi Jumamosi Januari 5, 2013. Man City ilishinda 3-0.

Balotelli akitoka uwanjani baada yamechi yao dhidi ya Watford juzi
Ujue wewe tunakutegemea kule Italia... kocha wa Watford, Muitalia Gianfranco Zola akizungumza na Muitalia mwenzake Mario Balotelli wa Manchester City baada ya firimbi ya mwisho wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester, England juzi Jumamosi Januari 5, 2013. Man City ilishinda 3-0.

Balotelli kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya Watford juzi

Balotelli akipasha na Scott Sinclair
Balotelli akijiandaa kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Edin Dzeko katika dakika ya 70 dhidi ya Watford huku kocha wake Roberto Mancini (kushoto) akishuhudia

MARIO Balotelli amekuwa kitovu cha matukio ya utata ndani na nje ya uwanja tangu alipowasili Etihad Stadium mwaka 2010, huku la karibuni zaidi likiwa ni kukunjana na kocha Roberto Mancini wakati wa mazoezi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa straika mwenzake wa Manchester City, Carlos Tevez, ambaye yeye mwenyewe pia aligombana na kocha huyo msimu uliopita katika 'bifu' lililomshuhudia akikaanje ya michuano kwa miezi sita, matukio yanayomhusu Balotelli hayana tofauti na yanayowahusu wachezaji wengine katika timu nyingine.

"Aina hii ya matukio yamekuwa yakitokea katika klabu zote nilizopitia," straika huyo wa zamani wa Manchester United aliwaambia waandishi wa habari.

"Lakini hapa Man City macho daima yako kwetu, daima kwa Roberto na Mario. Hivyo dainma yanatoka nje, lakini mambo kama haya yanatokea kila mahala. Mario amekuwa akifanya vyema. Amekuwa akijitihidi kujaribu kubadilika.

"Hicho ndicho alichofanya akitokea kwenye ugonjwa na kuwa majeruhi, na ndicho ambacho amekuwa akijaribu kufanya.

"Najaribu kumsaidia Mario. Nazungumza naye ndani na nje ya uwanja. Nazungumza naye kabla ya 'fri-kiki' ambayo tunatakiwa kupiga, na namruhusu aipige ili kuinua hali yake ya kujiamini, ili mambo yawe poa kwake.

"Nimepitia katika kipindi kama chake, hivyo daima niko tayari kumsaidia na kuendelea kumsaidia ili asirudie makosa yale yale."

Tevez alifunga huku Balotelli akiingia kutokea benchi wakati Man City walipopata ushindi wa kujiamini wa magoli 3-0 dhidi ya Watford 3-0 na kusonga mbele katika raundi ya nne ya Kombe la FA Jumamosi.

No comments:

Post a Comment