Tuesday, January 1, 2013

TAZAMA MAPICHA YA YANGA WANAVYOJIFUA UTURUKI NA MANDHARI YA BONGE LA HOTELI WALILOFIKIA.. NI RAHA TU

Dah... huku kunatamanisha sana kubaki!  Kutoka kushoto ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Frank Domayo na Simon Msuva. Hapa wakipozi kwa picha wakati wa mazoezi ya timu yao ya Yanga nchini Uturuki jana Desemba 31, 2012. 

Hoteli walilofikia Yanga nchini Uturuki... ni maraha utamu!

Simba watatukoma mwaka huu... makocha wa Yanga, Razak Siwa (kushoto) na Ernst Brandts wakitafakari wakati vijana wao (hawapo pichani) wakiendelea kujifua jana Desemba 31, 2012.

Huku tukizubaa lazima tuwe masharo kwa sana... Cannavaro (kulia) na Razak Khalfan wa Yanga wakiwa kwenye uwanja wao wa mazoezi nchini Uturuki jana Desemba 31, 2012.

Kutoka kushoto ni dogo Rehani, Mbuyu Twite, George Banda, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wa Yanga wakiendelea kujifua kwenye kambi yao nchini Uturuki jana Desemba 31, 2012.

No comments:

Post a Comment