Tuesday, January 8, 2013

RONALDO MECHI 6 NJANO 6... KUIKOSA MECHI IJAYO

Ronaldo akisikitika baada ya kuonyeshwa kadi ya njano jana
Ronaldo akionyeshwa kadi ya njano dhidi ya Real Sociedad
Ronaldo akivaa kitambaa cha unahodha baada ya nahodha wa kudumu Iker Casillas kumtaka aendelee kukivaa wakati wa mechi yao ya Jumapili dhidi ya Real Sociedad.

KATIKA mechi dhidi ya Real Sociedad Jumapili, Cristiano Ronaldo alilimwa kadi nyingine ya njano na kuzifanya kuwa tano msimu huu katika ligi, jambo linalomaanisha kwamba atafungiwa kucheza mechi moja. 

Straika huyo wa Real Madrid, ambaye jana usiku aliangushwa kwa mara ya nne mfululizo na Lionel Messi katika kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia, hatacheza mechi ijayo dhidi ya Osasuna Jumamosi.

Cristiano Ronaldo sasa amelimwa kadi za njano sita katika mechi sita mfululizo, na hii ni mara ya kwanza tangu alipotua Hispania kutumikia adhabu ya kadi tano. Kufikia sasa adhabu alizotumikia ni za kupewa kadi nyekundu za moja kwa moja.

Straika huyo Mreno ataweka kuweka nguvu zake kwa ajili ya kucheza mechi ya Jumatano ya Kombe la Mfalme, wakati Real Madrid watakapolazimika kugeuza matokeo ya kipigo cha 2-1 walichopata kutoka kwa Celta de Vigo katika mechi yao ya awali ugenini, na kisha ajifue zaidi kwa ajili ya mechi yao ngumu ya ugenini dhidi ya Valencia.

Kwa mara ya kwanza, katika  mechi rasmi ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo alivaa kitambaa cha unahodha, ingawa aliwahi kuwa nahodha siku za nyuma katika mechi ya kirafiki lakini. Alikuwa hawajawi kuvaa kitambaa cha unahodha katika mechi za ligi, kombe la mfalme wala Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Hata hivyo, alimpelekea kitambaa chake Casillas, wakati alipoingia uwanjani katika dakika ya sita kufuatia kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kipa Antonio Adan, lakini Iker hakukipokea akamuachia aendelee kukivaa.

Mchezaji mwingine ambaye hatacheza dhidi ya Osasuna ni kipa Antonio Adan, ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumuangusha ndani ya boksi straika Carlos Vela katika dakika ya sita.Wafungaji wanaoongoza La Liga:


Mchezaji Magoli Penalti
Lionel Messi Lionel Messi
Straika
Barcelona
27 2
Radamel Falcao Radamel Falcao Straika
Atlético de Madrid
17 6
Cristiano Ronaldo Cristiano Ronaldo Straika
Real Madrid
16 4
Aritz Aduriz Zubeldia Aritz Aduriz Zubeldia Straika
Bilbao
11 1
Rubén Castro Rubén Castro Straika
Betis
10 0

No comments:

Post a Comment