Monday, January 7, 2013

RONALDO AWEKA NAMBA ZA MAFANIKIO YAKE KWENYE KIATU CHAKE... AVAA KIATU KIMEANDIKWA "1-9-14-19-27-55-60" KWENYE MECHI NA SOCIEDAD

Ronaldo akishangilia baada ya kuwatungua Barca
Kiatu cha CR chenye namba 1-9-14-19-27-55-60

CRISTIANO Ronaldo alionekana akiwa amevaa kiatu kipya cha Nike CR Mercurial IX kwa mara ya kwanza jana katika mechi dhidi ya Real Sociedad kwenye Uwanja wa Bernabeu.

Kiatu hicho kimeorodhesha mafanikio yote ya Cristiano ya msimu wa 2011-12, kwenye namba 1-9-14-19-27-55-60 zilizoandikwa kwa pembeni.

Namba 1 inamaanisha taji lake la kwanza la La Liga, 9 na 14 zinamaanisha magoli (9)aliyofunga katika mechi (14) alizoichezea timu yake ya taifa, 19 inamaanisha rekodi yake mpya kuwa mtu wa kwanza katika historia ya La Liga kuzifunga timu zote 19 wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Hispania, 27 ni umri wake, 55 ni idadi ya mechi za kimashindano alizocheza msimu huo akiwa na Madrid na 60 ni idadi ya magoli aliyoifungia Real katika michuano yote.

No comments:

Post a Comment