Ronaldo akifunga penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Getafe jana. |
Messi akifunga goli lake la nne na la tano kwa Barcelona dhidi ya Osasuna jana |
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga goli la pili la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013. |
Cristiano Ronaldo (katikati) wa Real Madrid akifunga goli la tatu la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013. |
Messi akimfungisha tela mtu |
Safari hiyo... Lionel Messi akipita katikati ya wachezaji wa Osasuna |
Lionel Messi wa FC Barcelona akiondoka na mpira wake baada ya kufunga magoli manne katika mechi dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Hispania Januari 27, 2013. |
MECHI ya El Classico ya nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme baina Real Madrid na Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumatano itakuwa ni balaa kufuatia matokeo ya jana timu hizo mbili kubwa Hispania.
Real Madrid waliianza siku ya Jumapili mapema kwa ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Getafe, ambayo kwa mara nyingine tena ilishuhudia Cristiano Ronaldo akiwa katika kiwango chake cha juu kabisa cha kufunga mabao.
Ronaldo alifunga 'hat trick' dhidi ya mahasimu wao wa mji wa Madrid huku magoli yote matatu yakija katika kipindi cha pili.
Ulikuwa ni ukurasa mwingine wa msimu mzuri kwa Mreno huyo. Na namna ambayo Ronaldo alifunga 'hat trick' hiyo ni lazima pia izingatiwe: Goli moja alifunga kwa mguu wa kushoto, jingine mguu wa kulia na la tatu kwa kichwa. 'Hat trick' iliyokamilika kabisa kama ilikuwapo nyingine kama hiyo.
Magoli yote matatu ya Ronaldo yalikuja ndani ya dakika 10 tu na ilikuwa ni 'hat trick' yake ya 20 maishani na ya 19 akiwa na Real Madrid.
Idadi hiyo inafanya sasa Ronaldo awe amefunga jumla ya magoli 179 katika mechi 176 tangu alipotua misimu mitatu na nusu iliyopita akitokea Manchester United na imemuweka katika Na.6 ya wafungaji vinara wa zama zote klabuni hapo akiwa amemfikia gwiji wa zamani Francisco Gento. Kwa magoli 10 ambayo tayari ameyafunga mwaka huu pekee wa 2013, Ronaldo yuko katika kasi ya kuyafikia magoli ambayo Lionel Messi alifunga mwaka 2012 na kuvunja rekodi.
Lakini walisema kila Ronaldo analolifanya, Messi hulifanya vizuri zaidi na ilikuwa hivyo pia jana.
Messi jana aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya La Liga kufunga katika mechi 11 mfululizo wakati alipofunga magoli manne katika ushindi wa Barcelona wa 5-1 dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Nou Camp baadaye jana.
Muargentina huyo sasa amefikisha magoli 33 katika mbio za kuwania tuzo ya 'Pichichi' ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Hispania akifuatiwa na Ronaldo aliyefikisha magoli 22 baada ya 'hat trick' yake dhidi ya Getafe.
Messi sasa amefikisha jumla ya mabao 202 katika La Liga na kuwa mmoja wa wachezaji saba tu waliovuka magoli 200 katika Ligi Kuu ya Hispania.
Osasuna inaonekana kuwa ni timu ambayo Messi "anapenda" kuifunga baada ya kifunga jumla ya magoli 14 katika mechi 13 aliziocheza dhidi yao.
Hii ni mara ya tatu kwa Messi kufunga magoli manne katika mechi moja ya ligi, mara nyingine mbili zikija katika msimu wa kipekee kwake, alipofunga dhidi ya Valencia na Espanyol.
No comments:
Post a Comment