Yoan Gouffran |
NEWCASTLE imemsajili straika Yoan Gouffran kutoka Bordeaux.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye amesaini mkataba wa miaka minne kwa ada ya uhamisho ambayo haitajwi, amekuwa mchezaji mpya wa tatu kutua klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili cha Januari baada ya kusajiliwa pia kwa Wafaransa wenzake Mathieu Debuchy na Mapou Yanga-Mbiwa.
"Najivunia kujiunga na klabu hii bab'kubwa," Gouffran aliiambia tovuti rasmi ya Newcastle.
Straika huyo alikuwa kinara wa mabao wa Bordeaux akifunga magoli 12 katika mechi 27 za klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Ufaransa msimu huu.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya U-21 ya Ufaransa ametua kuziba pengo la Demba Ba, ambaye alikuwa kinara wa mabao kwa magoli 13 kabla hajaondoka mwezi huu kutua Chelsea, na atavaa jezi Na.11.
Kuwasili kwa Gouffran kunaifanya idadi ya wachezaji wa Kifaransa kufikia wanane klabuni St James' Park, ingawa wapo pia wachezaji zaidi wanaouzungumza Kifaransa akiwamo Msenegal Papiss Cisse, Mehdi Abeid na Cheick Tiote.
Winga wa Newcastle, Sammy Ameobi aliandika katika ukurasa wake wa Twitter juzi: "Nahitaji kujiboresha Kifaransa changu kwa sababu sasa inakuwa ni wazimu lol".
Wachezaji Wafaransa klabuni Newcastle sasa ni:
1. Yohan Cabaye
2. Hatem Ben Arfa
3. Mathieu Debuchy
4. Mapou Yanga-Mbiwa
5. Romain Amalfitano
6. Sylvain Marveaux
7. Gabriel Obertan
8. Yoan Gouffran
No comments:
Post a Comment