Hapa ni wakati wa kusomwa dua kabla jeneza la marehemu Sajuki halijapelekwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo Januari 4, 2013. |
Mhe. Zitto Kabwe (mwenye kanzu na barghashia) akikaribishwa msibani na watu wa bongomovie. kulia ni msanii Jissu.(PICHA ZOTE: Kwa Hisani ya issamichuzi.blogspot.com) |
Wasdanii wenzake mbalimbali nyota wa filamu, wanamuziki, viongozi mbalimbali wa kisiasa na wananchi wa kawaida ni miongoni mwa watu waliojitokeza ambapo baada ya swala ya Ijumaa na kisha mwili wa marehemu huyo ambaye jina lake kamili ni Juma Kilowoko, ulsafirishwa kutoka Tabta hadi kwenye makaburi ya Kisutu na kuzikwa kwa kufuata taratibu zote za Kiislamu.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mhe. Zitto Kabwe, ni miongoni mwa wanasiasa kibao walioshiriki mazishi hayo. Zitto ambaye pia ni mkazi wa Tabata na aliyeshiriki kwa kiasi kikubwa harakati za kumchangia Sajuki wakati akiugua kwa kuongoza kampeni maalum akishirikiana na wabnunge wezake kama Ester Bulaya (CCM) na Halima Mdee (Chadema), alionekana kivingine leo ambapo alitupia kanzu na kofia ya balaghashee vilivyomtoa na kuonekana kama sheikh fulani hivi wa ukweee!
No comments:
Post a Comment