Tuesday, January 29, 2013

LULU ACHEKA DAKIKA MOJA.... KISHA AMKUMBATIA MAMA YAKE NA KUMWAGA MACHOZI MFULULIZO KWA FURAHA HUKU ASIAMINI KUWA KWELI KAACHIWA KWA DHAMANA KATlULU IKA KESI INAYOMUANDAMA YA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA... AONDOKA KORTINI NA MGARI WA KISASA AINA TOYOTA LAND CRUISER

Lulu akifurahi baada ya kuachiwa kwa dhamana leo
Lulu akijibu maswali ya waandishi baada ya kuachiwa kwa dhamana leo

Lulu akilia baada ya kuachiwa kwa dhamana leo huku akisaidiwa na muigizaji mwenzake, Dokta Cheni, ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwezesha kutoka kwake kwa kipindi chote cha miezi tisa aliyokaa rumande binti huyo

Lulu akijibu maswali ya waandishi baada ya kuachiwa kwa dhamana leo

Lulu akimkumbatia mama yake mzaz Lucrecia Kalugila

Lulu akimkumbatia mama yake mzaz Lucrecia Kalugila

Mungu mkubwa... mama wa Lulu akifurahi baada ya mwanae kuachiwa kwa dhamana leo

Utatoka tu...! Lulu na akiwa na wanasheria wake na askari magereza.


Pole sana...!

Siamini! Lulu akiwa na Cheni (kulia)



Siamini...! Ndugu mmojawapo wa Lulu akilia kwa furaha hadi kudondosha simu yake.

Mama yake Lulu, Lucrecia akiwa na wanasheria wa binti yake

Lulu, mwanasheria wake na askari magereza.

Lulu akionekana mwenye mawazo tele kabla ya kupata dhamana leo.

Lulu, mama yake, Cheni na dada yake

Wanalia? Ni kilio cha furaha!



Lulu alionekana akicheka kwa furaha ya kuachiwa huru kwa dhamana kwa dakika chache leo alasiri akiwa na mama yake Lucrecia Kalugila, lakini muda mrefu baadaye wakajikuta wakibubujikwa na machozi bila breki ikiwa ni matokeo ya kuzidiwa na hisia za furaha hiyo huku pia wakionekana kutoamini juu ya kile kilichotokea.

Msanii huyo nyota wa filamu nchini, ameachiwa kwa dhamana hatimaye baada ya kutimiza masharti aliyiopewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika kesi inayomkabili ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake nyota, marehemu Steven Kanumba.

Awali, mama huyo wa Lulu, ndugu, jamaa, marafiki na wasanii mbalimbali wa filamu nchini walionekana mahakamani tangu saa 2:30 asubuhi jana, lengo likiwa ni kujua hatma ya mpendwa wao ambaye amekuwa akisota mahabusu tangu Aprili mwaka jana.

Baadaye, mama huyo alionekana kujawa na hisia kali kiasi cha kumwaga machozi yatokanayo na furaha aliyokuwa nayo baada ya mahakama kumuachia binti yake kwa dhamana na wote wawili kuonekana wakikumbatiana; kama watu wasioamini juu ya kile kilichotokea.

ILIVYOKUWA
Lulu mwenye miaka 18, anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake, Kanumba (28), aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa.

Msanii huyo alifikishwa saa 7:50 mchana akitokea mahabusu ya gereza la Segerea, akiwa katika ‘deffender’ jeupe la Magereza lenye namba za usajili STK 2823.

Mawakili wa pande zote walihakiki nyaraka za dhamana. Ilipofika saa 9:10 alasiri, Lulu alipandishwa kizimbani akiwa na wadhamini wake.

Mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Francis Kabwe, Lulu aliwawakilisha na wadhamini wawili, James Mboneka kutoka Wizara ya Afya na Florian Mutafungwa wa Wizara ya Ardhi.

Saa 9:20, Lulu alikamilisha taratibu za mahakama na kuachiwa huru hatimaye ambapo mama yake (Lucrecia), ndugu, jamaa na marafiki zake walijikuta wakiangua kilio cha furaha.

Akizungumza baada ya kuwa huru kwa dhamana, Lulu alisema anamshukuru Mungu pamoja na watu wote walio pamoja naye katika kipindi chote kigumu.
"Sina la kusema... nawashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi tangu nilipopata kesi hii. Ila bado nawaomba waendelee kuniombea kwa sababu nimepata dhamana tu, bado nina safari ndefu. Kesi  bado mbichi, niombeeni jamani," alisema Lulu huku akilia kabla ya kuondoka kwenye viunga vya mahakama hiyo akiwa ndani ya
gari lenye namba za usajili T 480 CFX, Toyota Land Cruser (V8) la rangi ya kijivu.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema dhamana ni mchakato wa kisheria unaotakiwa kufuatwa katika mahakama na kwamba mteja wao amefanikiwa kupata dhamana na sasa wanasubiri wito wa mahakama wakati itakapopanga tarehe kwa ajili ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri wa kesi ya msingi.
Mapema Juzi, Jaji Zainabu Mruke alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa huyo baada ya wakili wa utetezi Peter Kibatala kuwasilisha maombi ya dhamana kwa hati ya dharula chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (1) na cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).

Jaji Mruke alisema kosa linalomkabili  mshakiwa lina dhamana kisheria na kwamba mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kufuata masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali watakaosaini  hati ya dhamana ya Sh. milioni 20 kila mmoja.

Alitakiwa pia awasilishe hati zake za kusafiria, kuripoti kila tarehe Mosi ya mwezi kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha msajili huyo.
Katika kesi ya msingi, Lulu anadaiwa kuwa  Aprili 7, 2012, katika eneo la Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, alimuua Kanumba bila kukusudia.

No comments:

Post a Comment