Monday, January 14, 2013

AZAM YAPONGEZWA UBINGWA KOMBE LA MAPINDUZI

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeupongeza uongozi wa klabu ya Azam kwa timu yao kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, imesema Azam kwa kufanikiwa kutetea ubingwa huo inaonesha jinsi klabu hiyo ilivyojipanga kabla ya kuingia katika mashindano hayo ambapo ilicheza fainali dhidi ya Tusker FC ya Kenya.

"Ushindi huo utakuwa changamoto kwa timu nyingine za Tanzania Bara zitakazopata fursa ya kushiriki michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi mwakani," ilisema taarifa hiyo.

Michuano hiyo iko kwenye Kalenda ya Matukio ya TFF.

No comments:

Post a Comment