Wednesday, December 19, 2012

STOPILLA SUNZU: SIENDI ARSENAL JAMANI… NAENDA READING YA LIGI KUU YA ENGLAND AMBAYO INATAKA KUNISAJILI NA SIYO MAJARIBIO KAMA ANAVYOTAKA KOCHA WENGER WA ARSENAL…!

Stopilla Sunzu (kulia) akiwa na washkaji zake jijini Lusaka, juzi. 
Beki nyota wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo”,  Stopilla Sunzu amesema kuwa ameamua kwenda kuichezea klabu ya Reading inayoshiriki Ligi Kuu ya England na sio Arsenal  kwa sababu kocha Arsene Wenger amemueleza kuwa ni lazima afuatiliwe kwa muda mrefu zaidi kabla ya kupewa mkataba.

Beki huyo mwenye miaka 23,  ambaye amepaa kwenda Ghana pamoja na kocha Herve Renard na Rainford Kalaba kuhudhuria hafla ya kesho ya utoaji wa tuzo za wanasoka bora wa mwaka za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), amekaririwa na vyombo vya habari vya Zambia akisema kwamba amepata mwaliko kutoka Reading na kwamba, safari yake ya kwenda England imeiva.

“Nitasafiri kwenda England baada ya mechi yetu dhidi ya Tanzania lakini sitakwenda Arsenal. Arsenal wanataka nijaribiwe kwanza,” alisema Sunzu kabla hajaondoka kwenda Accra, Ghana jana.”

“Badala yake, nitakwenda Reading ambako nitasajiliwa tu na siyo kufanyiwa majaribio.

No comments:

Post a Comment