Friday, December 21, 2012

'SORRY' RONALDO, MESSI NDIYE No.1, ASEMA GIGGS

Ryan Giggs
Cristiano Ronaldo

Lionel Messi

VETERANI wa Manchester United, Ryan Giggs amesema nyota wa Barcelona, Lionel Messi ni bora kuliko mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Ronaldo ataikabili Man United kwa mara ya kwanza tangu alipoihama mwaka 2009 baada ya jana timu hiyo kupangwa kuikabili Real Madrid katika mechi ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Lakini Giggs anaona kwamba mpinzani wake wa zamani Messi ndiye anayetisha duniani, si Ronaldo.

"Unapaswa kumfikiria Messi," alisema Giggs alipoulizwa ni mchezaji gani bora zaidi katika historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

"Kwa sasa amevunja rekodi zote. Yeye ni mmoja wa wachezaji bora kabisa waliopata kutokea maishani na ameshatwaa tuzo ya mwanasoka bora mara kadhaa.

"Nitamchagua Messi. Yeye ni mfungaji – anafunga magoli mengi sana – lakini pia anaichezesha timu yake.

"Anapika magoli mengi sana kwa wachezaji wenzake na kwa kuwa nilipata kukabiliana naye, ni ngangari sana. Ni vigumu kumnyang'anya mpira.

"Ana uwezo mkubwa wa kukokota mpira, anaweza kufunga magoli ya aina zote, mguu wa kushoto, wa kulia, vichwa. Ana aseti nyingi sana – ni ngumu, ngumu sana kumdhibiti."

No comments:

Post a Comment