Saturday, December 15, 2012

MIKOA SITA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI TWFA

Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora.

Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

No comments:

Post a Comment