Saturday, December 15, 2012

MIKE TYSON AKANUSHA "UPUUZI" KWAMBA ETI KAJIBADILI JINSIA NA KUWA MWANAMKE AITWAYE MICHELLE... ASEMA HIYO SI HABARI YA UONGO TU, BALI NI UPUMBAVU KWANI HATA WALIOMUONA UKUMBINI KATIKA PAMBANO LA KINA MANNY PACQUIAO JUMAMOSI ILIYOPITA WALIMSHUHUDIA WAZI KWAMBA YEYE NI MWANAUME NGANGARI KINOMA...!

Niko ngangari...! Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu duniani, Mike Tyson akionekana jukwaani kabla y kupimwa uzito kwa mabondia Manny Pacquiao na Juan Mauel Marquez waliopigana kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena Jumamosi iliyopita (Desemba 8 2012) mjini Las Vegas, Nevada.
Mambo? Mike Tyson akisalimia huku amezungukwa na warembo jukwaani kabla ya pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao na Marquez mjini Las Vegas Jumamosi iliyopita (Desemba 8, 2012) 
Tyson akiingia ukumbini na wanawe katika tamasha la filamu jijini Paris, Ufaransa Mei 16 , 2008.
Tyson na wanawe wakiwa Ufaransa Mei 16, 2008.
Mike Tyson na mkewe Lakiha Spicer wakiwa Warsawa nchini Poland, April 2012. 
Tyson na mkewe Lakiha Spicer. Hii ilikuwa Machi 2, 2011.
NEW YORK, Marekani
Bondia bingwa wa zamani wa dunia, Mike 'Iron' Tyson amekanusha uvumi kwamba amefanyiwa upasuaji wa saa 16 kubadili jinsia yake na kuwa mwanamke aliyejipachika jina la Michelle.

Baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari Tanzania na kwingineko barani Afrika 'viliingia mkenge' kwa kuripoti uzushi huo kuhusiana na kubadili jinsia kwa Tyson na pia sura yake.

Chanzo cha taarifa hizo ambazo Tyson ameziita kuwa za kipumbavu ni tovuti iitwayo NewsBiscuit, iliyozichapisha mwishoni mwa Novemba.

Baadaye ikaripotiwa na gazeti la Jumapili la Zimbabwe. Tovuti ya Zambia Watchdog ikaidaka stori hiyo Jumatatu na kudakwa na tovuti ya SpyGhana Jumanne.

"Tumekuwa na wasomaji kutoka Afrika katika siku chache zilizopita kama tulivyotarajia kwa mwezi mzima," John O'Farrell wa tovuti ya NewsBiscuit aliiambia BBC, akiongeza kwamba habari hiyo ilisomwa zaidi ya mara 50,000.

Taarifa iliyodaiwa kutolewa na Iron Mike na kukaririwa na tovuti ya Spy Ghana ilisema: "Mimi bado ni mwanaume na siku zote nimekuwa mwanaume rijali na sijawahi kuwa na nia ya kutaka kuwa mwanamke. Madai hayo siyo tu kwamba ni ya uongo, bali ni upumbavu. Nilikuwapo ukumbini Jumamosi kushuhudia pambano la ngumi kati ya Pacquiao na Marquez na mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kueleza wazi kwamba niliyeonekana sikuwa mwingine bali mwanaume wa shoka."

No comments:

Post a Comment