Sunday, December 16, 2012

MESSI AMBWAGA VIBAYA RONALDO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA WA MWAKA WA JARIDA LA WORLD SOCCER

Lionel Messi

Cristiano Ronaldo

Andres Iniesta
Vicente Del Bosque

Jose Mourinho

LIONEL Messi ameibuka kuwa mshindi asiye na maswali wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka 2012 wa jarida la World Soccer. Nyota huyo wa Barcelona na Argentina alipata kura zaidi ya mara mbili ya walizopata wapinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Ureno, na mchezaji mwenzake wa Barca, Andres Iniesta wa Hispania.

Hii ni mara ya tatu kwa Messi kushinda tuzo hiyo, baada ya kuibeba pia mwaka 2009 na 2011. Ameungana na Mbrazil, Ronaldo Lima, ambaye alikuwa mchezaji pekee aliyeibeba tuzo hiyo mara tatu.

Kulikuwa pia na tuzo iliyotambua mafanikio ya aina yake ya timu ya taifa ya Hispania katika kushinda ubingwa wa Euro 2012. Vicente Del Bosque aliibuka na ushindi wa kishindo wa tuzo ya Kocha Bora wa Dunia wa Mwaka, na timu ya taifa ya Hispania ilitwaa tuzo ya Timu Bora ya Dunia ya Mwaka.

Mwaka huu, ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 30 ya tuzo hizo, kura za wasomaji zilijumuishwa na zile za jopo maalum la wataalam. Kura za mwisho (ambazo zimewekwa katika asilimia) zilikuwa zikipimwa kwa kuhakikishia kwamba asilimia 50 zinatokana na kura za wasomaji na asilimia 50 kutoka kwa jopo la majaji.

Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka 2012

1. Lionel Messi (Barcelona & Argentina) 47.33%

2. Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Ureno) 19.01

3. Andres Iniesta (Barcelona & Hispania) 9.77

4. Andrea Pirlo (Juventus & Italia) 6.10

5. Radamel Falcao (Atletico Madrid & Colombia) 5.95

6. Neymar (Santos & Brazil) 3.60

7. Iker Casillas (Real Madrid & Hispania) 2.30

8. Xavi (Barcelona & Hispania) 1.78

9 Didier Drogba (Chelsea/Shanghai Shenhua & Ivory Coast) 1.77

10 Eden Hazard (Lille/Chelsea & Ubelgiji) 0.37



Kocha Bora wa Dunia wa mwaka 2012

1. Vicente Del Bosque (Hispania) 28.49

2. Jose Mourinho (Real Madrid) 12.27

3. Roberto Di Matteo (Chelsea) 12.05

4. Jurgen Klopp (Borussia Dortmund) 10.33

5. Diego Simeone (Atletico Madrid) 7.19

6. Herve Renard (Zambia) 6.83

7. Marcelo Bielsa (Athletic Bilbao) 5.74

8. Tite (Corinthians) 4.67

9. Pep Guardiola (Barcelona) 2.72

10. Luis Tena (Mexico Olympic) 2.63



Timu Bora ya Dunia ya Mwaka 2012

1 Hispania 47.36

2 Zambia 8.52

3 Chelsea 7.84

4 Juventus 7.36

5 Atletico Madrid 4.89

6 Borussia Dortmund 4.25

7 Corinthians 4.23

8 Universidad de Chile 4.00

9 Barcelona 3.63

10 Montpellier 2.90



Mchanganuo wa kura

KURA ZA WASOMAJI
Mchezaji


Lionel Messi 40.13 %

Cristiano Ronaldo 18.94

Radamel Falcao 10.99

Andrea Pirlo 9.48

Neymar 7.20

Andres Iniesta 6.82

Xavi 2.65

Didier Drogba 2.63

Eden Hazard 0.76

Yaya Toure 0.38

Kocha

Del Bosque 21.54

Jose Mourinho 15.45

Roberto Di Matteo  11.38

Marcelo Bielsa 10.57

Jurgen Klopp 9.77

Tite 9.35

Diego Simeone 8.94

Herve Renard 7.31

Rene Girard 4.06

Luis Tena 1.63

Timu


Hispania 32.00

Juventus 12.00

Zambia 9.78

Chelsea 9.33

Atletico Madrid 8.88

Corinthians 8.45

Universidad 8.00

Borussia Dortmund 5.78

Montpellier 4.00

Mexico Olympic 1.78



KURA ZA MAJAJI

Mchezaji


Lionel Messi 54.54%

Cristiano Ronaldo 19.09

Andres Iniesta 12.73

Iker Casillas 4.54

Andrea Pirlo 2.73

Mohamed Aboutrika 0.91

Sergio Ramos 0.91

Radamel Falcao 0.91

Didier Drogba 0.91

Juan Mata 0.91

Zlatan Ibrahimovic 0.91

Xavi 0.91


Kocha

Vincente Del Bosque 35.45

Roberto Di Matteo 12.73

Jurgen Klopp 10.90

Jose Mourinho 9.09

Herve Renard 6.36

Diego Simeone 5.45

Pep Guardiola 5.45

Antonio Conte 3.64

Luis Tena 3.64

Roberto Mancini 1.81

Cesare Prandelli 1.81

Alex Ferguson 0.91

Rene Girard 0.91

Jorge Sampaoli 0.91

Theo Bucker 0.91

Marcelo Bielsa 0.91
 

Timu

Hispania 62.73

Zambia 7.27

Barcelona 7.27

Chelsea 6.36

Real Madrid 5.45

Borussia Dortmund 2.73

Juventus 2.73

Montpellier 1.81

Al Ahly 0.91

Manchester United 0.91

Atletico Madrid 0.91

Bayern Munich 0.91

Manchester City 0.91


---------

No comments:

Post a Comment