Friday, December 7, 2012

MESSI: NIKO POA KABISA, NAWEZA KUCHEZA J'PILI, ASANTE KWA NYOTE MLIONISAPOTI

Messi akiumia kwa kugonga goti kwenye kwapa la kipa wa Benfica, Artur Moraes wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambayo ilimalizika kwa sare ya 0-0.
Mbishi... Licha ya kuumia Messi bado alimpita kipa na kujaribu kufunga lakini kipa alirudi haraka na kudaka mpira huo.

Kisha akakaa chini kusikilizia maumivu
Akajaribu kuinuka....
Lakini wapi bhana, akarudi chini....

Kisha akalala chini kabisa....

Mbio mbio madaktari wakawahi...

Wasiwasi wako tu kijana. Mi sioni kama una tatizo kubwa hapa
Hebu panda kwenye hiki kigari tukakupime freshi...
Usijali jembe... rekodi ya Gerd Muller utaifikia tu... kwani si umebakisha goli moja tu?


NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amesema anajisikia yuko poa kabisa baada ya kuhofiwa kuumia goti katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica Jumatano.

Messi alitolewa kwa machela baada ya kugongana na kipa wa Benfica, Artur Moraes, lakini presha zilishuka baada ya uthibitisho kutolewa muda mfupi baadaye kwamba maumivu hayakuwa mabaya zaidi ya mchubuko tu kwenye goli lake la kulia.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikuwa akijifua kwenye gym wakati wachezaji wenzake wakifanya mazoezi uwanjani jana, na Messi alisema bado ipo nafasi ya yeye kucheza mechi yao ya Jumapili.

"Najisikia vyema, lakini sijui kama nitakuwa tayari kucheza mechi ya Jumapili," alisema katika tukio la promosheni kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. "Nitaona. Nina faraja kwa meseji zote na sapoti niliyopata."

Messi alisema aliumia wakati alipogongana na Moraes, lakini alijaribu kufunga kwa shuti la mkunjo wa ndizi kabla ya kuanguka "sakafuni" huku akiwa ameshikilia goti lake.

"Nilidhani kwamba lingekuwa shuti langu la mwisho hadi baada ya muda mrefu sana," alisema. "Hivyo nikaamua kucheza kamari kwa kupiga mpira langoni."

Aliongeza: "Ukweli ni kwamba sikufikiria chochote kwa sababu nilichokuwa nacho pale ni maumivu tu. Lakini kwa wakati ule nilidhani ni majeraha mabaya. Nilipoambiwa kwamba si makubwa nikatulia."

No comments:

Post a Comment