Saturday, December 22, 2012

MESSI AFUNGA LA 91, BARCA YAZIDI KUPAA

Xavi Hernandez (katikati) wa FC Barcelona akishangilia na wachezaji wenzake Lionel Messi (kushoto) na Jord Alba baada ya kufunga dhidi ya Real Valladolid kwenye Uwanja wa Jose Zorrilla mjini Valladolid, Hispania leo Desemba 22, 2012. Barca walishinda 3-1.

Lionel Messi (kulia) wa Barcelona akimfungisha tela Victor Perez wa Valladolid wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa Jose Zorrilla mjini Valladolid, Hispania leo Desemba 22, 2012. Barca walishinda 3-1.

BARCELONA wameshinda mechi yao ya 16 kati ya 17 za La Liga msimu huu baada ya kuilaza Valladolid 3-1 kwenye Uwanja wa Jose Zorilla usiku huu, huku Lionel Messi akifunga goli lake la 91. 

Huku kocha Tito Vilanova akiwa anaendelea vyema baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutibu kansa ya koo, kocha msaidizi Jordi Roura aliongoza jahazi leo katika mechi ambayo wageni walitawala mwanzo-mwisho. Xavi alifunga goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya Lionel Messi kuongeza la pili katika dakika ya 60. 

Javi Guerra alifanya mambo yawe magumu kwa Barca wakati alipoipatia Valladolid goli moja katika dakika za lala-salama, lakini Christian Tello aliyeingia katika dakika ya 94 alifunga goli la tatu kwa kutumia mpira wake wa kwanza kugusa uwanjani na mechi ikamalizika.

No comments:

Post a Comment