Friday, December 21, 2012

KOCHA WA ZAMBIA ATWAA TUZO YA CAF YA KOCHA BORA WA AFRIKA MWAKA 2012... ZAMBIA YATWAA TUZO YA TIMU BORA YA MWAKA... KUTUA DAR NA KINA FELIX SUNZU, RAINFORD KALABA KUIVAA TAIFA STARS J''MOSI

Kocha wa Zambia, Herve Renard akibebwa juujuu na wachezaji wake baada ya kutwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2012) mwanzoni mwa mwaka huu nchini Gabon. 
ACCRA, Ghana
Kocha wa Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya CAF YA Kocha Bora wa Afrika 2012 huku timu yake pia ikitwaa Tuzo ya CAF ya Timu Bora ya Mwaka 2012.

Renard na timu yake ya Zambia wametangazwa washindi usiku huu (Desemba 20, 2012) katika utoaji wa tuzo hizo jijini Accra, Ghana.

Zambia maarufu kama 'Chipolopolo', walitwaa tuzo hiyo baada ya kuzishinda timu za mataifa ya Cape Verde na Ivory Coast.

Zambia walitwaa taji lao la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2012) mwanzoni mwa mwaka huu nchini Gabon na  Equatorial Guinea baada ya kuonyesha kiwango cha juu na kuifunga Ivory Coast kwa penati katika mechi yao ya fainali iliyoanza kwa kuchezwa dakika 120 bila kushuhudia nyavu zikitikisika.

Wakati huo huo, kocha Renard anatarajiwa kwenda moja kwa moja jijini Dar es Salaam na kuungana na kikosi chake cha timu ya taifa kinachojiandaa kwa mechi yao ya ugenini Jumamosi (Desemba 22, 2012) dhidi Tanzania 'Taifa Stars'.

Renard atatua jijini Dar es Salaam na nyota wake Stopilla Sunzu na Rainford Kalaba ambao waliambatana na kocha huyo nchini Ghana kwavile nao walikuwa wakiwania tuzo malimbali za CAF; ambapo Topilla Sunzu (23), alikuwa Ghana kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.

No comments:

Post a Comment