Friday, December 28, 2012

JOSE MOURINHO ATUA DUBAI NA KUSEMA HUU SIYO WAKATI WA KUJADILI HATMA YAKE REAL MADRID... KUKUTANA NA MARADONA, RADAMEL FALCAO, PLATINI

Mourinho (kushoto) akipokewa na wenyeji wake baada ya kutua katika uwanja wa ndege jijini Dubai jana.
DUBAI, Falme za Kiarabu
José Mourinho alitua jijini Dubai jana kushiriki katika mkutano wa saba wa michezo wa kimataifa (Dubai International Sports Conference).

Wakati akiwasili, kocha huyo wa Real Madrid aliulizwa kama ana mpango wa kuendlea kubaki na klabu yake ya sasa. Akajibu: "Sasa si wakati wa kuzungumzia hatma yangu", aliwaambia waandishi wa habari huku akitabasamu.

Mourinho ni miongoni mwa vinara wanaonogesha mkutano huo akiwa pamoja na Diego Armando Maradona, ambaye ndiye mwenyeji, rais wa UEFA, Michel Platini, ambaye ndiye mfunguaji wa mkutano na straika wa klabu ya Atlético de Madrid, Radamel Falcao.

1 comment:

  1. JOSE MOURINHO is a good and great football coach.Recently come in Dubai meets authority and a big deal both of them.

    ReplyDelete