Monday, December 17, 2012

JOSE MOURINHO AKIRI REAL MADRID HAIWEZI TENA KUIKAMATA BARCELONA NA KUPIGANIA TAJI LA LA LIGA MSIMU HUU... NI BAADA YA KUSHIKILIWA KWA SARE YA 2-2 KATIKA MECHI WALIYOTAWALA DHIDI YA ESPANYOL...!

MADRID, Hispania
Hatimaye kocha Jose Mourinho wa Real Madrid amerusha taulo na kusema kuwa timu yake haiwezi tena kukwea kileleni mwa msimamo wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kutetea taji lao msimu huu.

Mourinho amekubali yaishe baada ya timu yake kushikiliwa kwa sare isiyotarajiwa ya 2-2 kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu jana huku mahasimu wao Barcelona ambao wako kilelelni mwa ligi hiyo wakiibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Atletico Madrid.

"Sijawahi kuwa katika nafasi kama hii, kupoteza pointi kibao. Tutajaribu kumaliza msimu vizuri kadri tutakavyoweza. Tutapigania mataji lakini la ligi kuu linaonekana kwetu kuwa haliwezekani," amesema Mourinho.


Matokeo ya mechi za jana zilizokuwa za raundi ya 16 yameifanya Real Madrid iachwe na vinara Barcelona kwa tofauti ya pointi 13.

No comments:

Post a Comment