Sunday, December 23, 2012

CHELSEA YATOA KIPIGO CHA MSIMU... MAN UTD YAVUTWA SHATI

Frank Lampard wa Chelsea akishangilia kufunga goli lao la nne katika mechi yake ya 500 kuanza katika Ligi Kuu ya England dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England leo Desemba 23, 2012. Chelsea iliua 8-0.
Christian Benteke (kushoto) na Ashley Westwood (15) wa Aston Villa wakiwa wamejawa na fadhaa baada ya kichapo kutoka kwa Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012. Chelsea ilishinda 8-0. 

Mshambuliaji Christian Benteke (kulia) na Jordan Bowery wa Aston Villa wakionekana kusawijika baada ya kufungwa magoli 8-0 wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012.

Eden Hazard wa Chelsea akishangilia na Victor Moses baada ya kufunga goli lao la saba wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England  dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012. Chelsea ilishinda 8-0.

Eden Hazard wa Chelsea akishangilia na Victor Moses baada ya kufunga goli lao la saba wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England  dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012. Chelsea ilishinda 8-0.

Eden Hazard wa Chelsea akishangilia na David Luiz baada ya kufunga goli lao la saba wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England  dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012. Chelsea ilishinda 8-0.

Ramires wa Chelsea (kulia) akishangilia na Oscar na Victor Moses baada ya kufunga goli lao la nane wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London, England Desemba 23, 2012.
Patrice Evra wa Manchester United akifunga goli dhidi ya Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea nchini Wales jana Desemba 23, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1.

Patrice Evra wa Manchester United akishangilia goli alilofunga dhidi ya Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea nchini Wales jana Desemba 23, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1.

Patrice Evra wa Manchester United akishangilia goli alilofunga dhidi ya Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea nchini Wales jana Desemba 23, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1.

Patrice Evra wa Manchester United akishangilia goli alilofunga dhidi ya Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea nchini Wales jana Desemba 23, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1.

Patrice Evra wa Manchester United akishangilia goli alilofunga dhidi ya Swansea City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Liberty mjini Swansea nchini Wales jana Desemba 23, 2012. Timu hizo zilitoka 1-1.


CHELSEA walicharuka kwa staili ya aina yake na kuisambaratisha kabisa Aston Villa iliyo katika kiwango cha juu na kurejea katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, huku vinara Manchester United wakishikiliwa katika sare ya 1-1 dhidi ya Swansea.

Fernando Torres aliendeleza kasi yake ya kufufua makali chini ya kocha wa Blues, Rafael Benitez kwa kufunga goli tamu la kichwa katika dakika ya tatu tu ya mchezo.

Na goli jingine zuri la 'fri-kiki' iliyokwenda moja kwa moja wavuni kutoka kwa David Luiz likafanya matokeo yawe 2-0 kabla ya kichwa cha Branislav Ivanovic kuwapeleka Chelsea mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 3-0. Torres sasa amefunga magoli 7 katika mechi 6 zilizopita chini ya kocha wake wa zamani aliyemfanya atishe klabuni Liverpool, Benitez.

Frank Lampard alisherehekea mechi yake ya 500 akiwa na Chelsea kwa kufunga goli la shuti la mbali katika dakika ya 60 na magoli mawili kutoka kwa Ramires, penalti ya Oscar na goli la juhudi binafsi kutoka kwa Eden Hazard yalikamilisha kipigo hicho cha mbwa-mwizi.

Pamoja na uthibitisho wa Chelsea kufufuka chini ya Benitez, kipigo hicho kiliweka rekodi za Ligi Kuu ya England.

Matokeo hayo yaliweka rekodi ya kuwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya England kwa wachezaji saba tofauti wa timu moja kufunga katika mechi moja na pia iliifikia rekodi ya Chelsea ya kushinda magoli mengi zaidi kama iliposhinda 8-0 dhidi ya Wigan Mei 2010.

Kikosi cha Villa ambacho hakikubadilishwa kilienda katika mechi hiyo kikiwa katika kiwango cha juu huku kikitokea kuishangaza Liverpool kwa kuichapa 3-1 Jumamosi iliyopita.

Kipigo hicho kimekuwa ndicho kikubwa zaidi kwa Aston Villa katika ligi kuu. Waliwahi kulala 7-0 mara tano huku kipigo cha karibu zaidi cha idadi hiyo ya mabao kikija mwaka 1950.


Manchester United wanaenda katika Sikukuu ya Krismasi wakiongoza kwa tofauti ya pointi 4 baada ya sare ya kufadhaisha ya 1-1 ugenini dhidi ya Swansea.

Kichwa cha Patrice Evra kiliwapa Man United goli la kuongoza kutokana na kocha ya Robin van Persie, lakini Swansea walijibu mapigo kupitia kwa kinara wa mabao Michu aliyefunga kiulaini baada ya shuti la Jonathan De Guzman kupanguliwa mbele yake na kipa David De Gea.

Man U waligongesha nguzo za goli mara mbili baada ya mapumziko, na Van Persie alicharuka kwa hasira wakati shuti la Ashley Williams lilipompiga kisogoni wakati akiwa amelala 'sakafuni'.

Williams aliosha mpira katika dakika ya 74 na ukampiga kisogoni Van Persie, ambaye alinyanyuka kutaka kumkunja beki huyo, na wote wakalimwa kadi za njano.

Van Persie alikaribia kuifungia timu yake goli la ushindi wakati shuti lake lilipogonga besela na mchezaji mwenzake Michael Carrick pia kichwa chake kiligonga nguzo ya lango.

Ilikuwa ni sare ya kwanza kwa Man United, ambao wameweza kutoruhusu goli mara nne tu msimu huu na ambao wamefungwa magoli 25, lakini safu yao kali ya ushambuliaji imekuwa ikiwaokoa.  


Nafasi Timu Mechi Goal Difference Pointi
1 Man Utd 18 19 43
2 Man City 18 19 39
3 Chelsea 17 19 32
4 Arsenal 18 14 30
5 Everton 18 8 30
6 Tottenham 18 5 30
7 West Brom 18 4 30
8 Liverpool 18 4 25
9 Stoke 18 2 25
10 Norwich 18 -7 25
11 Swansea 18 4 24
12 West Ham 18 0 23
13 Fulham 18 -5 20
14 Newcastle 18 -6 20
15 Sunderland 18 -5 19
16 Aston Villa 18 -17 18
17 Southampton 17 -11 15
18 Wigan 18 -15 15
19 QPR 18 -16 10
20 Reading 18 -16 9

No comments:

Post a Comment