Friday, November 9, 2012

UCHAGUZI TAREFA, TAFCA SASA DESEMBA 22


UCHAGUZI wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA) na Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) sasa utafanyika Desemba 22 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba za uchaguzi za vyama hivyo, kamati zao za uchaguzi zitatangaza kuanza mchakato wa uchaguzi Novemba 10 mwaka huu wakati fomu kwa wanaotaka kugombea uongozi zitaanza kutolewa Novemba 12 mwaka huu. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Novemba 16 mwaka huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa mwongozo huo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA baada ya kuomba hivyo kutokana na wagombea sita tu kujitokeza kuomba nafasi tatu za uongozi katika mchakato wa awali.

Kwa waombaji ambao awali walichukua na kulipia ada ya fomu za kugombea uongozi TAFCA na TAREFA, hawatatakiwa kulipia tena ada kwa nafasi zile zile walizoomba, isipokuwa watatakiwa kujaza fomu upya.

No comments:

Post a Comment