Thursday, November 29, 2012

SCOLARI KOCHA MPYA BRAZIL, CARLOS ALBERTO PARREIRA AWA MKURUGENZI WA UFUNDI

Luiz Felipe Scolari

LUIZ Felipe Scolari alitangazwa kuwa kocha mpya wa wenyeji wa Kombe la Dunia 2014 Brazil leo, akirejea kuifundisha nchi yake kwa mara ya pili katika jaribio la kutwaa ubingwa wao wa sita kwenye ardhi ya nyumbani katika muda wa chini miezi 18.

Kocha huyo ambaye pia hufahamika kama Felipao (Big Phil), ambaye aliiongoza Brazil kutwaa taji lao la tano na la mwisho la dunia katika fainali za mwaka 2002, alitambulishwa rasmi na Shirikisho la Soka la Brazil kwenye mkutano na waandishi wa habari, akichukua nafasi iliyoachwa na Mano Menezes aliyetimuliwa Ijumaa iliyopita.

Carlos Alberto Parreira, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa ubingwa wao wa nne wa dunia mwaka 1994, alitangazwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wakati shirikisho hilo la soka la Brazil likijaribu kurekebisha kugeuza muda.

Scolari (64) alisema yuko tayari kwa changamoto za kudili na 'presha' na matarajio ya Wabrazili wenzake milioni 190.

"Najisikia mwenye hamasa, kijana, najiona naweza," aliuambia mkutano na waandishi wa habari.

"Tuna mtihani wa kutwaa ubingwa; hatupewi nafasi kwa sasa lakini tunadhamiria kupewa nafasi wakati wa michuano. Nafasi ya tatuy ama ya nne haitoshi kwa timu ambayo imetwaa Kombe la Dunia mara tano."

Kutambulishwa kwa Scolari na Parreira kumekuja siku mbili tu kabla ya kupangwa kwa ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho, ambalo pia litafanyikia nchini Brazil.

Mechi ya kwanza ya Scolari madarakani itakuwa ni ya kirafiki ugenini dhidi ya England Februari.

No comments:

Post a Comment