Sunday, November 25, 2012

REAL MADRID YAZAMISHWA TENA... BARCA WANAWEZA KUWAPITA KWA POINTI 11 WAKISHINDA LEO


Benzema akijilaumu katika mechi ya jana waliyolala 1-0 ugenini dhidi ya Real Betis
REAL Madrid walipata pigo kubwa kileleni mwa msimamo usiku wa kuamkia leo baada ya kulala 1-0 kwa Real Betis kwenye Uwanja wa Estadio Benito Villamarin, na kuziweka mbio zao za kuwania kutetea ubingwa matatani.

Benat alifunga goli pekee la mechi hiyo, akitupia kutokea nje ya ya eneo la penalti baada ya makosa katika safu ya ulinzi wa Real Madrid, ambao, licha ya kupeleka presha kubwa katika kipindi cha pili, walishindwa kupita katika timu "iliyopaki basi" ya wenyeji na kuwapandisha hadi nafasi ya nne ya msimamo.

Kikubwa katika matokeo hayo, ni kwamba kama vinara wa Barcelona wataibuka na ushindi dhidi ya Levante leo Jumapili, Madrid walio katika nafasi ya tatu, watajikuta wakiachwa kwa pointi 11 nyuma ya Wacatalunya, huku mechi ngumu dhidi ya wapinzani wa jadi Atletico Madrid ikija wiki ijayo.

Jose Mourinho alifabadili mchezaji mmoja tu kutoka katika kikiosi kilichotoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City katikati ya wiki, huku Mesut Ozil akiingia badala ya Luka Modric.

Wenyeji walipata goli lao katika dakika ya 17 baada ya Benat kuupokea mpira vizuri nje ya ukingo wa boksi na kufumua shuti lililoenda kutinga kwenye kona ya chini ya lango - goli lililofuatia Angel Di Maria kupoteza mpira.

Baada ya kosa kosa nyingi za timu yake, Mourinho mwanzoni mwa kipindi cha pili aliwaingiza Khedira na Ozil na kuwatoa Modric na Kaka lakini haikusaidia kuwaokoa mabingwa na kipigo cha tatu katika mechi za ligi msimu huu.

Karim Benzema alifunga goli lililoonekana kuwa safi kabisa lakini likakataliwa kwa madai ya kuotea na pia Real walinyimwa penalti.

Wafungaji wanaoongoza Ligi Kuu ya Hispania

Magoli Penalti
Lionel Messi Lionel Messi
Straika
Barcelona
17 1
Cristiano Ronaldo Cristiano Ronaldo
Straika
Real Madrid
12 4
Radamel Falcao Radamel Falcao
Straika
Atlético de Madrid
10 4
Aritz Aduriz Zubeldia Aritz Aduriz Zubeldia
Straika
Bilbao
8 1
Negredo Negredo
Straika
Sevilla
7 2

No comments:

Post a Comment