Friday, November 9, 2012

M'VILA AFUNGIWA TIMU YA TAIFA UFARANSA HADI 2014

Yann M'Vila

KIUNGO wa timu ya taifa ya Ufaransa, Yann M'Vila amefungiwa kuchezea timu zote za taifa hilo hadi Juni 2014 baada ya kutoka usiku kwenda kujirusha bila ya ruhusa wakati akiwa katika timu ya taifa ya vijana ya Under-21.

M'Villa (22) ameichezea timu ya taifa ya wakubwa mara 22 na alikuwa akiwindwa na Arsenal na Tottenham katika kipindi kilichopita cha usajili.

Kifungo chake kinamaanisha kwamba atakosa fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kama Ufaransa itafuzu.

Wachezaji wengine wanne - Wissam Ben Yedder, Antoine Griezmann, Chris Mavinga na M'baye Niang - wamefungiwa hadi Desemba 31, 2013.

Kiungo wa ulinzi wa Rennes, M'Vila alifungiwa mechi moja kwa kukataa kumpa mkono kocha wa wakati huo Laurent Blanc wakati alipopumzishwa katika mechi yao dhidi ya Hispania katika fainali za Euro 2012.

Shirikisho la Soka la Ufaransa limefanya maamuzi hayo baada ya wachezaji watano kwenda kujirusha katika klabu ya usiku ya Paris katikati ya mechi mbili za kuwania kufuzu kwa fainali za Euro za Under-21 dhidi ya Norway ambazo Ufaransa ililala kwa jumla ya magoli 5-4.

No comments:

Post a Comment